IQNA

Ustaarabu wa Kiislamu

Maajabu ya Usanifu Majengo: Haram ya Imam Ridha (AS) ni ya aina yake

11:41 - September 17, 2023
Habari ID: 3477614
MASHHAD (IQNA) – Ninafumba macho yangu na mbele yangu naona Haram Takatifu (kaburi) yenye kubaa linalong’aa kwa utukufu wakati machweo yanapoingia.

Hili ni kaburi kubwa la lenye kuba la dhahabu ni la Imam Ridha (AS) Imam wa nane wa Shia.

Kila mwaka mamilioni ya wafanyaziara husafiri hadi mji wa Iran wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa mkoa wa Khorasan Razavi kuzuru eneo hilo takatifu.

Mkurugenzi Haram Takatifu ya ImaM Ridha (AS), Mustafa Feizi, alisema Jumatano kwamba kwa wastani wafanyaziyara wapatao elfu 400 hutembelea eneo takatifu kila siku.

Idadi hiyo, alisema, inaongezeka hadi milioni 1.4 katika hafla maalum za kidini.

Mwaka huu wa 1435 Hijria Qamari, Siku ya Jumamosi ambayo ni siku ya mwisho ya Safar, sanjari na kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Ridha (AS) wafanyaziara takribani milioni 4.5 kutokana Iran na maeneo yote duniani walizuri eneo hilo takatifu.

Imam Ridha (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), alizaliwa Madina mwaka 148 Hijria Qamaria na alihamia Iran baada ya amri ya Mamun, khalifa wa saba wa ukoo wa Bani Abbas.

Huu ulikuwa ndio wakati sehemu muhimu zaidi ya maisha yake kuhusu jukumu lake la kisiasa na kidini ilipoanzishwa na kuhitimishwa na kifo chake cha kishahidi mwaka 203 Hijria Qamaria.

Kutokana na hadhi ya Imam Ridha miongoni mwa Waislamu kaburi lake tukufu lilikuwa moja ya vitovu vya kidini kwa Waislamu na hasa wa madhehebu ya Shia. Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) Imekuwa na maendeleo makubwa ya usanifu majengo katika historia yake yote.

An Architectural Wonder: Imam Reza Holy Shrine Is A Masterpiece

Haram tukufu ya Imam Ridha (AS) imeshuhudia maendeleo makubwa ya ujenzi katika kipindi  chatakriban miaka elfu moja. Imekuwa ikikaratabitwa kila mara, na imedumishwa na ujenzi na upanuzi  katika  enzi tofauti.

Mchanganyiko mzuri ni udhihirisho safi wa sanaa za Kiislamu.

Haram ya Imam Ridha (AS) ni moja ya sehemu muhimu za kidini kwa Wairani na Waislamu kote ulimwenguni.

Kwa mujibu wa Shirika la Elimu, Utamaduni na Sayansi  la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Kumpfer, mtalii wa Ujerumani ambaye alitembelea Iran wakati wa (1096-1105 Hijria/ 1685-1694 Miladia) analitaja eneo hilo takatifu kuwa bora na la kipekee.

“Katika majengo matakatifu na bora zaidi, pana na yanayovutia zaidi nchini Iran, bila shaka, kwanza ni Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad. Pili, kaburi Takatifu la dada yake huko Qom na, tatu, kaburi la Sheikh Safi al-din Khanegah huko Ardabil, "alisema.

An Architectural Wonder: Imam Reza Holy Shrine Is A Masterpiece

UNESCO inasema mji wa Mashahd uliibuka kutokana ujenzi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS),  kwa hivyo, kaburi hilo takatifu linakuwa kituo cha kidini, kisiasa, kijamii na pia kisanii cha jiji hilo.

Pia, kwa kiasi kikubwa eneo hilo takatifu, huathiri hali ya kiuchumi ya jiji, inasema.

"Urithi huu wa usanifu, kwa sababu ya ujenzi wake wa muda marefu, vipengee vya mapambo kama vile vigae, mapambo ya vioo, kuba iliyopambwa kwa rangi, kazi za mawe, kazi za plasta, n.k. hujumuisha thamani kuu zinazoonekana na zisizoonekana."

Kwa mujibu wa UNESCO, kuba la Allah-Verdikhan, kuba la Hatam Khani, Shule ya Do Dar, Shule ya Parizad na majengo mbalimbali ya kihistoria kama vile minara, Saqqa khanehs (nyumba za maji), Neqareh Khanehs, n.k., pamoja na vitu vya makumbusho na maandishi katika Ofisi wa Mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha (AS) ni kati ya vipengele vingine vya thamani katika eneo hilo takatifu.

Pia UNESCO inasema kuwa Msikiti wa Gowharshad, ambao sasa ni sehemu ya Haram ya Imam Ridha (AS) ni wa usanifu muhimu wa kihistoria ndani ya mjumuiko wa majengo ya eneo hilo takatifu.

Msikiti huo unachukuliwa kuwa kazi bora ya usanifu majengo wa Kiirani wakati wa silsila ya watawala wa Teimurian kwa sanaa yake nzuri ya mapambo na vigae.

Mbunifu mashuhuri wa wakati wa Teimurian, Qavam al-din ibn Zein al-din Shirazi alijenga jengo hilo kwa kutumia matofali na jasi kwa mtindo wa usanifu majengo halisi wa Kiislamu.

An Architectural Wonder: Imam Reza Holy Shrine Is A Masterpiece

Iran imewasilisha pendekezo kwa UNESCO  kuipa hadhi ya turathi ya dunia kwa Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) kama eneo la kiroho linalotembelewa na waumini kutoka duniani kote.

Pendekezo hilo likiidhinishwa, UNESCO itasaidia katika kuhifadhi mila ya ziyara katika eneo hilo takatifu  ambayo imekita mizizi katika imani za Waislamu wengi duniani.

Habari zinazohusiana
captcha