IQNA

Mashhad

Mashhad tayari kukaribisha Mamilioni ya Mahujaji wakati wa likizo ya Nowruz

17:02 - March 04, 2023
Habari ID: 3476655
TEHRAN (IQNA)-Maandalizi yanaendelea katika mji mtakatifu wa Mashhad, kaskazini-mashariki mwa Iran, kupokea kwa furaha mamilioni ya wafanyaziara wanaopanga kutembelea jiji hilo wakati wa likizo ya Nowruz yam waka mpya wa Hijria Shamsia (kuanzia Machi 21).

Haya ni kwa mujibu wa Mohsen Davari, gavana wa Mashhad, ambaye alisema siku ya Jumamosi kwamba makao makuu yameanzishwa ili kuratibu juhudi za kuwahudumia mahujaji.

Mahujaji wote watakaribishwa katika sehemu za kuingilia iwe wanasafiri kwa nchi kavu, kwa ndege au kwa gari moshi, alibainisha.

Afisa huyo aliongeza kuwa usimamizi wa hoteli na kituo cha malazi umeimarishwa ili kuhakikisha watatoa huduma zinazostahiki.

Mashhad ni makao ya kaburi takatifu au Haram ya Imam Ridha (AS), Imam wa 8 wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia na mjukuu wa Mtume Muhammad SAW. Ni moja ya vituo vya Ziyara vinavyotembelewa zaidi ulimwenguni.

Makumi ya mamilioni ya wafanyaziyar kutoka kote Iran pamoja na nchi nyingine hutembelea mji huo mtakatifu kila mwaka.

Ni mojawapo ya maeneo yanayopendwa sana na Wairani wakati wa likizo ya Nowruz ambayo inaashiria mwanzo wa Mwaka Mpya wa Hijria Shamsiya.

4125880

Kishikizo: mashhad nowruz
captcha