IQNA

Ahadi ya Kweli

Nukta nane kuhusu Shambulio la Kulipiza kisasi la Iran dhidi ya Israel

20:22 - April 16, 2024
Habari ID: 3478691
IQNA - Mchambuzi wa Lebanon ameorodhesha nukta nane kuhusu mashambulizi ya kulipiza kisasi wa Iran dhidi ya utawala haramu wa Israel ambayo yalikuja baada ya mashambulizi ya Israel kwenye ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria.

Tarehe 1 Aprili, utawala wa Israel ulifanya shambulizi la kigaidi dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria Damascus. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa jengo la ubalozi linachukuliwa kuwa ni ardhi ya nchi inayomiliki ubalozi huo.

Shambulio hilo la Israel lilisababisha kuuawa shahidi Brigedia Jenerali Mohammad Reza Zahedi, kamanda wa ngazi za juu katika Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Quds (IRGC), naibu wake, Jenerali Mohammad Hadi Haji Rahimi, na maafisa watano walioandamana nao, ambao wote walikuwa Syria kisheria kama washauri wa kijeshi..

Katika kulipiza kisasi shambulizi hilo, IRGC ililenga Israel Jumamosi kwa msururu wa ndege zisizo na rubani na makombora. Shambulio hilo la kulipiza kisasi, lililopewa jina la Operesheni ya Ahadi ya Ukweli, limesababisha uharibifu katika kambi za jeshi la Israel katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu.

Baada ya kulipiza kisasi, Iran iliwasilisha ujumbe kwamba inachukulia swala hilo kama lililomalizika na pia kuonya kwamba itatoa jibu kubwa na kali zaidi kikiwa utawala wa Israel  au washirika wake watalenga Iran.

Katika makala kwa IQNA, mchambuzi wa kisiasa wa Lebanon Hossein Ali Rezq ametaja nukta nane kuhusu shambulizi la kulipiza kisasi la Iran dhidi ya Israel

1) Iran imeweka wazi kwamba shambulio lolote katika eneo lake, iwe ndani ya mipaka yake ya kijiografia au katika vituo vyake vya kidiplomasia, ni mstari mwekundu.

2) Iran ilionyesha uwezo wake wa kijeshi, kijasusi na kidiplomasia kwa kuvurumisha ndege zake zisizo na rubani na makombora dhidi ya Israel na kushambulia ngome ndani ya Israel. Hatua hiyo ya Iran imechukuliwa hata baada ya kuonywa kuwa eti adui amejiandaa kwa mfumo wa hali ya juu wa mifumo ya ulinzi wa anga. Hata baadhi ya mataifa yenye nguvu za kijeshi duniani (ikiwemo Marekani, Uingereza, Ufaransa, na nchi kadhaa za Kiarabu) yalijulishwa mapema kuhusu hujuma ya Iran ambapo ndege zisizo na rubani za Iran zilitumia saa 2-3 kabla ya kutua Israel. Pamoja na hayo waitifaki hao wa Israel walishindwa kukabiliana na wimbi kubwa la hujuma ya Iran.

Kwa mtazamo wa kidiplomasia, Iran ilijizuia kwa siku chache, na kutoa nafasi kwa ulimwengu na Baraza la Usalama kulaani shambulio dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran jijini Damascus. Iran ililazimika kujibu mashambulizi ya utawala wa Israel chini ya Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kwa kujilinda.

3) Wairani waliweza kuidhalilisha Israel na washirika wake kwa kutangaza moja kwa moja operesheni zao za kijeshi. Katika siku za nyuma, Israel ilitia chumvi wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa shambulio la Iran. Hata hivyo, shambulio hili lilizidi walivyotarajia Waisraeli.

4) Iran ilifanikiwa kuanzisha vita vya kisaikolojia dhidi ya Israel. Iliiweka serikali ya utawala huo, raia wake, na wafuasi wake katika tahadhari ya hali ya juu, ikiingiza hali ya woga na wasiwasi. Utawala wote ulikuwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa shambulio la makombora. Inafaa kutaja hapa  kuwa Iran haikutumia uwezo wake wote wa kimkakati wa mapigano katika shambulio lake.

5) Wairani walianzisha mashambulizi huru bila ya msaada wowote wa washirika wake katika mhimili wa muqawama huko Lebanon, Yemen, au Iraq. Hii inadhihirisha kuwa Iran ina uwezo wa kutosha kukabiliana na wapinzani wake na haihitaji msaada kutoka kwa washirika wake.

6) Iran iliweza kusambaratisha vitisho kutoka kwa nchi za Magharibi hasa Marekani. Kwa upande mwingine, pia ilizuia pande zinazopingana kuchukua hatua zozote za kulipiza kisasi.

7) Iran ilijibu mashambulizi kwa kutumia chaguo moja tu, bila ya haja ya kuchukua hatua nyingine kama vile kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz, kulenga maeneo nje ya Israel, au kutafuta usaidizi kutoka kwa washirika wake.

8) Shambulio la Iran liliwakilisha mabadiliko katika stratijia yake ya miaka 45. Sasa kutokana na hatua hiyo ya Iran, taswira potovu ya kutoweza kutandikwa Israel imevunjwa, jambo ambalo limeufedhehesha kwa utawala huo.

3487964

captcha