IQNA

Turathi za Kiislamu

Msahafu wa zama za Uthmaniyya wauzwa kwa dola 144,000 katika mnada London

11:19 - April 27, 2024
Habari ID: 3478742
IQNA – Msahafu wa kipekee wa zama za Uthmaniyya umeuzwa katika katika mnada wa turathi za Kiislamu jijini London, Uingereza.

TMsahafu huo umepigwa mnada katika kupiga mnada cha Sotheby's London katika mnada athari za sanaa ya Kiislamu na Kihindi ambazo zimekusanywa kwa zaidi ya miaka 40. Nakala hiyo adimu ya Qur'ani Tukufu imeuzwa kwa dola 144,000 ikiwa ni rekodi katika mnada huyo uliofanyika ALhamisi.

Nakala hiyo ya Qur'ani ya zama za Uthmaniyya iliagizwa na Munire Sultan, binti ya Sultan Abdulmejid wa Kwanza wa Utawala Uthmaniya, na iliandikwa na mtaalamu wa kaligrafia  Ibrahim Hakki. Tarehe iliyoandikwa katika msahafi huo mo 19 Rabi' I 1277 Hijria Qamaria (Oktoba 5, 1860 MIladia) na inaonyesha tamaduni tajiri za kisanii za Ufalma wa Uthmaniyya.

Nakala hiyo ina kipimo cha sentimita 37.9 kwa 26.4 na inajumuisha kurasai 256. Kila ukurasa una mistari 15 ya hati maridadi ya naskh, iliyoainishwa vyema kwa dhahabu.

Wataalamu wa Sotheby awali walikadiria bei ya mnada ya Msahafu huo wa kipekee kuwa kati ya $86,700 na $111,400.

3488093

captcha