IQNA

UNESCO yalaani uchokozi wa Israel katika Msikiti wa al Aqsa

23:08 - October 21, 2015
Habari ID: 3391462
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekosoa uchokozi wa wazi wa utawala haramu wa Israel katika ardhi za Wapalestina unazozikalia kwa mabavu hasa katika msikiti wa al Aqsa ulio katika mji Quds au Jerusalem.

Wanachama wa taasisi hiyo muhimu ya UN wamepitisha azimio linalolaani hatua ya Israel ya kuwazuia Waislamu kufika katika msikiti mtakatifu wa al-Aqsa. Azimio hilo pia limekosoa utawala ghasibu wa Israel kwa kushindwa kuwalinda Waislamu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Nchi 6 ambazo ni Marekani, Uingereza, Ujerumani, Jamhuri ya Czech , Astonia na Uholanzi zimepinga azimio hilo huku nchi 26 zikipiga kura ya kuliunga mkono.

Utawala ghasibu wa Israel umewaua shahidi Wapalestina wasiopungua 45 katika kipindi cha majuma matatu yaliyopita baada ya kuanzisha uchokozi mpya huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Tukufu.

3391442

captcha