IQNA

Mitetemeko Uturuki na Syria

Waislamu katika eneo la Balkan wakusanyika kusaidia walioathirika na mitetemeko Uturuki

23:35 - February 09, 2023
Habari ID: 3476539
TEHRAN (IQNA) – Watu katika nchi za Balkan Magharibi za Kosovo na Macedonia Kaskazini wamejipanga kusaidia Uturuki baada ya mitetemeko ya ardhi yenye ukubwa wa 7.7 na 7.6. kupelekea karibu watu elfu 20 kupoteza maisha hadi sasa huku idadi kubwa yanyumba zikiwa zimeharibiwa Uturuki na Syria.

Katika msikiti wa Seydi Bey ulioko katika mji wa Prizren, ulioko kusini mwa Kosovo, jumuiya hiyo ilichangisha fedha kusaidia ndugu zao wa Uturuki, kufuatia maafa yaliyosababishwa na mitetemeko ya ardhi iliyoathiri mikoa 10.
Mufti wa Jimbo la Prizren Besim Berisha alitangaza kuwa zaidi ya €2,000 ($2,144) zimekusanywa kwa muda mfupi, huku wanawake pia wakichangia hereni na pete zao.
Berisha alisema euro 2,221, lira 100 za Kituruki, pete mbili za dhahabu, pete ya dhahabu na sarafu ya dhahabu zilikusanywa kwa mkupuo mmoja.
Wanafunzi wa Kituruki huko Skopje, mji mkuu wa Macedonia Kaskazini, pia walizindua kampeni ya kukusanya misaada ya kibinadamu kwa wahasiriwa wa tetemeko la ardhi nchini Uturuki.
Wanafunzi waliweka mahema katika uwanja wa Macedonia huku watu wakileta mahitaji ya kimsingi kama vile chakula cha makopo, blanketi, nguo, nepi na vinywaji baridi.
Kando na kampeni za kuchangisha fedha na mashirika yasiyo ya faida, misaada pia ilikusanywa katika Bazaar ya Kale ya Kituruki katika mji mkuu.
Katika Msikiti wa kihistoria wa Mustafa Pasha huko Skopje, mji mkuu wa Macedonia Kaskazini, Qur'ani ilisomwa pamoja na dua kwa ajili ya wale walioathiriwa na maafa hayo.
Mpango huo ulifanywa kwa ushirikiano na Umoja wa Kiislamu wa Macedonia Kaskazini, na Ushauri wa Huduma za Kidini wa Ubalozi wa Uturuki huko Skopje.

3482412

Kishikizo: uturuki mitetemeko
captcha