IQNA

Siku ya Quds ni nembo ya mapambano ya Umma wa Kiislamu

15:23 - April 28, 2022
Habari ID: 3475180
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds ni nembo ya muqawama au mapambano katika Umma wa Kiislamu.

Ayatullah Sadeq Amoli Larijani akisema hayo jana katika kikao cha halmashauri hiyo na kusisitiza kuwa, suala la Palestina na Quds tukufu ni kadhia nambari moja katika Umma wa Kiislamu hivi sasa. 

Amesema, Siku ya Quds ni nembo ya muqawama wa Umma wa Kiislamu na umma huo hivi sasa una jukumu la kulibainisha na kuliutangaza kwa upana zaidi suala hilo kuliko wakati mwingine wowote na kuuonesha ulimwengu upeo mkubwa wa busara za Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye ndiye aliyefanya ubunifu huo wa kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds.

Ijumaa ya kesho ya tarehe 29 Aprili 2022 ndiyo Siku ya Kimataifa ya Quds kwa mwaka huu wa 1443 Hijria.

Kabla ya hapo pia, msemaji wa Idara ya Mahakama ya Iran naye alikuwa ameashiria Siku ya Kimataifa ya Quds na kuitaja siku hiyo kuwa dhihirisho la umoja wa Umma wa Kiislamu kwa ajili ya kuukomboa mji mtakatifu wa Quds.

Zabihullah Khodaeian alisema hayo na kuongeza kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds haifungamani na dini au madhehebu maalumu bali ni siku ya wanadamu wote walio huru. Amesema, hiyo  ni siku ya kupambana na dhulma na ubaguzi wa rangi  na kuongeza kuwa, washiriki wa maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds watalaani jina za utawala wa Kizayuni wa Israel. 

4053147

captcha