IQNA

Kampeni ya Mshikamano na Palestina yazinduliwa Malaysia

17:19 - April 24, 2022
Habari ID: 3475163
TEHRAN (IQNA) - Katika kampeni iliyoitwa 'Hands Off Al-Aqsa Mosque' (Achaneni na Msikiti wa Al Aqsa), Baraza la Ushauri la Malaysia la Mashirika ya Kiislamu (Mapim) na mashirika 43 yasiyo ya kiserikali (NGOs) yameonyesha mshikamano wao na Wapalestina.

Mashirika yasiyo ya kiserikali yalilaani shambulizi la hivi majuzi la utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina katika msikiti huo wakati huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mashirika hayo yasiyo ya kiserikali kwa kauli moja yalionyesha uungaji mkono wao na kusimama kidete na Wapalestina wanaotetea Msikiti wa Al-Aqsa na maeneo mengine ya ibada katika Ardhi hiyo Tukufu.

Rais wa Mapim Azmi Abdul Hamid alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kujiunga na mshikamano na watu wa Palestina.

Amesema Wapalestina wanakabiliwa na mapambano makali katika kuulinda Al-Aqsa, msikiti wa tatu mtakatifu wa Kiislamu, kutokana na uvamizi wa Wazayuni.

Azmi alionya kuwa ghasia hizo zitasababisha mzozo zaidi. Alibainisha kuwa zaidi ya watu 200, wengi wao wakiwa Wapalestina, wamejeruhiwa katika mapigano ya hivi karibuni.

Azmi amesema utawala wa Kizayuni wa Israel kwa  unabeba dhima ya vile matokeo mabaya ya  kuwazuia Wapalestina kuingia katika Msikiti wa  Al-Aqsa, jambo ambalo lilizua mvutano uliosababisha mapigano.

Vile vile alisikitika kuwa baadhi ya mataifa ya Kiarabu yamejikurubisha kwa Israel na kuanzisha uhusiano na utawala huo huku wakipuuza masaibu yanayowapata ndugu zao Waislamu huko Palestina.

Makamu wa rais wa Angkatan Belia Islam Malaysia (ABIM) Ahmad Fahmi Mohd Shamsudin alisema kitendo cha Israel kukiuka sheria za kimataifa ndio chanzo cha mvutano wa hivi karibuni katika mji wa Quds (Jerusalem) uliko Msikiti wa Al Aqsa.

Ahmad Fahmi, ambaye pia ni afisa mkuu mtendaji wa Global Peace Mission (GPM), alisema serikali ya Malaysia inafanya iwezavyo kuongoza kwa mfano.

Waziri Mkuu wa Malaysia Ismail Sabri Yaakob amelaani vitendo vya wanajeshi wa Israel na kusema ni vya aibu na visivyo vya kibinadamu.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje Saifuddin Abdullah alieleza masikitiko yake kwamba mapigano hayo pia yalizuka siku ya Ijumaa, na wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Ahmad Fahmi pia aliitaka serikali ya Malaysia kuendelea kutetea ustawi wa Wapalestina.

Afisa mkuu na msemaji mkuu wa Wakfu wa Al-Quds wa Malaysia Dk Sharif Abu Shammalah amesema utawala wa Israel daima unajaribu kubadilisha utambulisho wa Msikiti wa Al-Aqsa, ikiwa ni pamoja na kubomoa miundo yake.

Lakini ana imani kwamba nchi zote zikiungana na kufanya kazi pamoja kuzuia vitendo vyao vya kinyama, hatimaye vitaleta matokeo chanya.

Utawala wa Kizayuni na Mayahudi wenye kufurutu mipaka huamini kuwa Msikiti wa Al Aqsa ni milki yao na hivyo kipaumbele cha kuingia katika msikiti huo mtakatifu kinapaswa kupewa Mayahudi. Ni kutokana na itikadi hiyo potovu ndio kunatekelezwa njama ya Kuuyahudisha Msikiti wa Al Aqsa na kupotosha historia sambamba na kupuuza haki za Wapalestina.

Ili kuweka mambo wazi , mwaka 2016, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) lilipasisha azimio na kusema Mayahudi hawahusiki kivyovyote vile na maeneo matakatifu ya Quds ukiwemo Msikiti wa al Aqsa. Azimio hilo la UNIESCO lilisema wazi kuwa, maeneo hayo matakatifu ni ya Waislamu. Aidha Kamati ya Nnne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Novemba 202 ilipasisha azimio ambalo liliungwa mkono na nchi 139 na kutangaza kuwa, Msikiti wa Al Aqsa una utambulisho kamili wa Kiislamu na hauna uhusiano wowote na Mayahudi.

3478623

captcha