IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Utawala wa Kizayuni uchukulie kwa uzito onyo kutoka Iran

21:09 - March 18, 2022
Habari ID: 3475048
TEHRAN (IQNA)-Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ameashiria shambulio la makombora la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) dhidi ya vituo vya ujasusi vya utawala wa Kizayuni huko Erbil, Iraq.

Hujjatul Islam Walmuslimin, Sayyid Mohammad Hassan Abu Turabi-Fard, amesema katika hotuba zake za Sala ya Ijumaa mjini Tehran kwamba amesema kwamba, wanasiasa wa Tel Aviv wanapaswa kuzingatia onyo zito la baadhi ya wanasiasa kwamba tahadhari ya Iran haipaswi kupuuzwa. 
Mapema Jumapili iliyopita vituo viwili vya Shirika la Ujasusi na Operesheni Maalumu la utawala wa Kizayuni wa Israel (Mossad) mjini Erbil, huko Kaskazini mwa Iraq, vimepigwa kwa makombora yaliyorushwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran.
Taarifa ya Idara ya Uhusiano wa Umma wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imesema: Kufuatia jinai za hivi karibuni za utawala bandia wa Israel, na tangazo la hapo awali na IRGC la kutonyamazia kimya jinai za utawala huo, jana usiku, "kituo cha kistratijia cha njama na uovu wa Wazayuni" kililengwa kwa makombora erevu ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Aidha Imamu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amezungumzia ukandamizaji wa utawala wa Al-Saud na mauaji ya halaiki ya makumi ya vijana nchini Saudi Arabia na kusema undumakuwili wa nchi za Magharibi kuhusu haki za binadamu ni mwanzo wa mwisho wa nguvu ya Magharibi na kuporomoka mfumo wa ubeberu.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia Jumamosi iliyopita iliwanyonga watu 81 kwa siku moja ikiwa ni katika hatua zake za kuendeleza ukikaji wa haki za binadamu nchini humo. Kati ya watu hao walionyongwa 41 ni vijana wa Kiislamu wa madhehebu Shia kutoka katika mji wa Qatif huko Mashariki mwa Saudia, 7 ni raia wa Yemen na mmoja ni Msyria; ambao walitiwa nguvuni na kufungwa jela na serikali ya Saudia kwa visingizio mbalimbali.  
Imamu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran, Hujjatul Islam Walmuslimin, Sayyid Mohammad Hassan Abu Turabi-Fard, amesema katika hotuba zake za Swala ya Ijumaa mjini Tehran kwamba hivi karibuni Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alifanya safari nchini Saudi Arabia kuunga mkono jinai za utawala wa ukoo wa Aal Saud na kuhoji kwamba, walimwengu wanapaswa kufanya nini hasa kuhusu sera na misimamo hii ya kindumakuwili?
Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa, "Ikiwa kweli unajali haki za binadamu, kwa nini umefanya safari katika nchi hiyo mara baada ya uhalifu huu wa kutisha ili kuonyesha uungaji mkono wako kwa utawala huo?"
Amesema undumakuwili wa nchi za Magharibi kuhusu haki za binadamu ni mwanzo wa mwisho wa nguvu ya Magharibi na kuporomoka mfumo wa ubeberu na kuongeza kuwa, hatua hiyo inakinzana na misingi ya awali ya haki za binadamuna na inashabihiana na vitendo vya zama za ujahilia. Abu Turabi-Fard amesema kuwa, hatua ya Waziri Mkuu wa Uingereza ya kuzuru Saudia baada tu ya mauaji hayo inapingana na sheria za kimataifa, misingi ya ubinadamu na kanuni zilizokubalika kimataifa.
Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjinii Tehran amewaonya wale ambao mikono yao imejaa damu safi ya watu wasio na hatia wajue kwamba, vitendo hivyo vya ukandamizaji vinawasha moto wa hasira ya Umma wa Kiislamu dhidi ya utawala huko Hijaz. 
4043975
 
 
 

captcha