IQNA

Wajue watafiti wa Qur'ani /40

Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy, mfasiri wa Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili

21:28 - January 24, 2024
Habari ID: 3478248
IQNA-Sheikh Abdullah al-Farsy, alikuwa mwanazuoni wa Kizanzibari mwenye asili ya Oman, na aliandika mojawapo ya tafsiri kamili za mwanzo za Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili.

Tafsiri yake imekuwa marejeo ya Waislamu wazungumzao Kiswahili Afrika Mashariki na maeneo yote duniani tangu ilipochapishwa miaka ya sitini. Sheikh al-Farsy aidha alikua ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Kiislamu duniani katika zama zake mbali na kuwa malenga na mwanahistoria.

Sheikh Farsy alizaliwa Zanzibar tarehe 12, Februari 1912 , katika familia yenye sifa ya kupenda na kutabahari katika elimu.

Mwaka mmoja kabla ya kuzaliwa kwake, Sultan Khalifa II bin Harub Al-Busaidi, sultani wa tisa wa Zanzibar kutoka familia ya al-Busaidi, alikuwa ameingia madarakani. Kipindi hicho kilikuwa enzi za utawala wa hekima na busara ambao Zanzibar ilishuhudia amani na maendeleo, licha ya matukio makubwa na migogoro katika maeneo mengine ya dunia, ikiwa ni pamoja na vita vikuu vya pili vya dunia na kuenea kwa ukomunisti, na mapambano dhidi ya ukoloni.

Masomo ya Qur'ani

Al-Farsy alipofikisha umri wa kwenda shule, baba yake alimpeleka kwa wanawake wasomi wa Kiislamu waliokuwa wakifundisha Qur'ani majumbani mwao, na akahifadhi Qur'ani katika shule hizo, kisha mwaka 1924 alijiunga na shule pekee ya msingi ya umma Zanzibar, ambayo ilifunguliwa mwaka 1904 wakati wa utawala wa Sultani. Ilianzishwa na Sultan Ali bin Hamoud Al Busaidi (1911-1902).

شیخ عبدالله الفارسی : نخستین مترجم قرآن به زبان سواحیلی

Katika skuli hii, pamoja na sayansi ya Kiislamu, alisoma masomo mapya, kaligrafia na Tajweed, kisha akajiunga na Chuo cha Ualimu Zanzibar. Katika kipindi hiki, Zanzibar ilishuhudia ufunguzi wa skuli mbali mbali, mafunzo ya kina ya walimu wa kufundisha katika skuli hizo, na pia kufunguliwa kwa skuli ya kwanza ya wasichana mwaka 1927. Kwa namna fulani, harakati hizo za kielimu na kitamaduni zilikuwa zikiendeshwa kwa msaada wa moja kwa moja wa Sultani wa wakati huo.

Kuhitimu

Baada ya kuhitimu kutoka Dar al-Mulammin, Al Farsi alifanya kazi ya ualimu na mwaka wa 1933, aliteuliwa kuwa mwalimu katika shule za msingi za umma za Zanzibar na kisha kuwa mkaguzi mkuu wa elimu za Kiislamu.

Baada ya muda, aliwahi kuwa mkurugenzi wa Chuo cha Kiislamu na kisha mkurugenzi wa shule ya Kiarabu katika kipindi cha 1952-1947. Kipindi ambacho kilikuwa ni miongoni mwa siku zenye tija kubwa katika maisha yake, ambapo alijishughulisha sana na masomo ya sayansi za Kiislamu,  lugha ya Kiarabu na kufasiri Qur'ani Tukufu , pamoja na kuandika maudhui za kihistoria na  vipindi vya mawaidha ya Kiislamu katika Radio Zanzibar na pia Mombasa nchini Kenya.

شیخ عبدالله الفارسی : نخستین مترجم قرآن به زبان سواحیلی

Baada ya hapo, alifanya kazi kama mhariri wa gazeti la al-Falaq na akachapisha mashairi yake mengi na makala za nathari ndani yake. Gazeti hili lilianzishwa mwaka 1929 na likaendelea kuchapishwa kwa miaka 35 na lilionekana kuwa moja ya magazeti muhimu sana Zanzibar na yenye ushawishi mkubwa katika kuandika habari za ndani na nje ya nchi.

Mapinduzi ya Zanzibar na kuelekea Kenya

Hata hivyo, baada ya mapinduzi ya Zanzibar na kisha kuanzishwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa kuwa hakuafiki sera za serikali mpya, hasa ukandamizaji wa watu wenye asili ya Oman, alijiuzulu na kuondoka Zanzibar mwaka 1964 na kuelekea nchi jirani ya Kenya.

Alikaribishwa Kenya na Sheikh Muhammad Kassim Al-Mazrui. Sheikh Al Farsy hakupata maarufu Kenya kama alivyokua Zanzibar. Pamoja na hayo, kutokana na ujuzui wake mkubwa wa mafundisho ya Kiislamu pamoja na umahiri katika lugha za Kiarabu, Kiswahili na Kiingereza alichaguliwa kama Kadhi Mkuu nchini Kenya na rais wa wakati huo, Jomo Kenyatta baada ya kupendekezwa na Sheikh Muhammad Kassim Al-Mazrui.

Sheikh Al Farsy alishikilia wadhifa huo kwa busara na hekima kwa muda wa miaka 14 hadi alipostaafu 1981 na kurejea katika nchi ya mababu zake, Oman.

Akiwa Oman, aliishi Muscat kwa miezi kadhaa na kisha aliaga dunia mwaka wa 1982.

Tarjama na tafsiri ya kwanza ya Qur'ani kwa Kiswahili

Moja ya kazi muhimu za Sheikh Abdullah Al Farsy ni tarjama na tafsiri ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili. Tafsiri hii ni miongoni mwa marejeo muhimu ya kidini na Qur'ani kwa Waislamu wanaozungumza Kiswahili katika Afrika Mashariki na duniani kote, na kinatajwa kuwa ni kazi kubwa ambayo imekuwa kizuizi kikubwa dhidi ya upotofu na mashambulizi dhidi ya imani ya Waislamu na Qur'ani Tukufu katika ulimwengu wa wazungumzao Kiswahili.

Ujuzi mkubwa wa Sheikh Abdullah Al Farsy katika sayansi  mbalimbali za Kiislamu kama vile tafsiri, historia na fiqhi na umahiri wake wa lugha za Kiarabu na Kiswahili zimeifanya tafsiri na tafsiri hii kuwa ya kipekee.

Book page image

Mapambano na Makadiani

Hadi kufikia mwishoni mwa miaka ya 1950, hapakuwa na tafsiri au tarjama sahihi ya Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili, na kwa miaka mingi wazungumzao Kiswahili walinyimwa ufahamu sahihi wa Qur’ani.

Tarjama  ya kwanza ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili ilikuwa ya Mchungaji Mmishonari "Godfrey Dale". Tarjama hii ilichapishwa mjini London mwaka 1923, na madhumuni yake yalikuwa ni kurahisisha mchakato wa kunukuu aya za Qur'ani kwa wamishenari wa Kikristo Afrika Mashariki na kukabiliana na wanazuoni wa Kiislamu katika mijadala mbalimbali katika eneo hili.

Ilikuwa mwaka wa 1953 ambapo Mirza Mubarak Ahmad Al-Ahmadi, kutoka pote la Kadiani, alichapisha tarjama na tafsiri ya Qur'an Tukufu kwa lugha ya Kiswahili huko Nairobi, ambapo mitazamo yake ilipingwa  wanazuoni wa Kiislamu Afrika Mashariki.

Tarjama na tafsiri ya Sheikh Abdullah al-Farsi ilikabiliana na itikadi potovu za Makadiani. Tafsiri hii, kwa mujibu wa watafiti wa historia ya Kiislamu katika Afrika Mashariki, imeendelea kuwa marejeo ya Waislamu na wanazuoni wa Qur'ani, na baada ya hapo, wafasiri daima wamemtaja Sheikh Abdullah al-Farsi kuwa Sheikhna al-Jalil na Sheikhna.

Mwanzoni mwa uchapishaji wa tafsiri hii, baadhi ya Makadiani walimtuhumu kuwa eti alitimua maelezo na tafsiri yao, Sheikh alibainisha kwa uwazi jambo hili na akakanusha tuhuma hii kwa kutaja sababu za kihistoria.

شیخ عبدالله الفارسی : نخستین مترجم قرآن به زبان سواحیلی

Sheikh Al Farsy alianza kuandika tafsiri yake mwaka wa 1956. Wakati huo kulishuhudiwa kupanuka kwa fikra potovu za  Kadiani huko Zanzibar hasa kuhusu mwisho wa utume, mwisho wa utume na masuala yanayohusiana na Umahdi. Mitazamo ya Makadiani kuhusu maudhui hizo inakinza na rai zinazokubaliwa na Waislamu kwa ujumla.

Sheikh Abdullah al-Farsy alijaribu kadri awezavyo katika tafsiri yake kujibu maswali yaliyoibuka. Juhudi hii ilifanikiwa na kuweza kukabiliana na wimbi la Makadiani wakati huo.

Faqihi, Mwalimu na Hakimu

Isisahaulike kuwa Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy pamoja na kazi yake kubwa ya tarjama na tafsiri ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili pia alikuwa ni mwalimu, faqihi na hakimu, na aliyaelewa vyema matatizo ya jamii ya Zanzibar na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kuanzia 1944 hadi 1964, alifundisha sayansi ya kidini na tafsiri ya Qur'ani Tukufu msikitini siku mbili kwa wiki na kila siku katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa miaka ishirini. Kwa hiyo, tafsiri yake ya Qur'ani ambayo imeandikwa kwa njia rahisi na inayoeleweka, na wakati huo huo ni sahihi na ya kina, inatokana na uzoefu wake wa miaka mingi katika kufundisha, kuhukumu, na pia kufanya kazi kama mwanachuoni wa kidini.

Sheikh Abdullah al-Farsy pia ameandika vitabu kwa lugha ya Kiingereza, na muhimu zaidi hapa tunaweza kutaja  "Al-Busaidi: The Rulers of Zanzibar". Kitabu hiki kinahusu historia ya utawala wa Masultani wa Oman wa silsila ya Al-Busaidi huko Zanzibar. Kitabu hiki kilitafsiriwa na kuchapishwa kwa Kiarabu na Abdullah Al Bastaki.

4195615

captcha