IQNA

Ulimwengu wa Kiislamu

OIC yaalani vikali hujuma za Wazayuni dhidi ya Msikiti wa al Aqsa

20:42 - April 24, 2023
Habari ID: 3476910
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali mashambulizi ya Wazayuni katika eneo la Babul Rahma katika Msikiti Mtakatifu wa al Aqsa.

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kwa mara nyingine tena katika siku ya Pili ya Sikukuu ya Idul-Fitr wameendeleza hujuma na mashambulizi yao katika eneo la Babul Rahma katika Msikiti Mtukufu wa al Aqsa na kufanya uharibifu mkubwa ambapo waliharibu njia ya umeme na kuvunja milango ndani ya eneo hilo ambalo ni sehemu muhimu isiyoweza kutenganishwa na Msikiti wa al Aqsa.   

Sekretarieti Kuu ya OIC imeyataja mashambulizi endelevu ya utawala wa Kizayuni dhidi ya matukufu ya Kiislamu na Kikristo huko Palestina hususan vitendo vya kuvunjia heshima na kufanya uharibifu katika eneo la Babul Rahma katika Msikiti wa al Aqsa kuwa vinakiuka sheria za kimataifa. 

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu pia imelaani kitendo cha Wazayuni cha kupandisha bendera ya Israel katika kuta za Haram ya Nabii Ibrahim na kukitaja kuwa ni ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya  Geneva na maazimio ya kimataifa na kwamba ni uchochezi wa hisia za Umma wa Kiislamu. 

OIC imesema, utawala wa Kizayuni wa Israel ndio unaopasa kubeba kikamilifu dhima ya aathira mbaya zinazosababishwa na mashambulizi mtawalia ya Wazayuni dhidi ya matukufu na raia wa Palestina; na imetaka jamii ya kimataifa iwajibike ili kuhitimisha uhalifu wa Israel ambao unaweza kusabababisha mapigano ya kidini na kuzusha machafuko katika eneo la Magharibi mwa Asia. 

3483321

Kishikizo: oic al aqsa israel
captcha