IQNA

Msikiti wa Al Aqsa

Sala ya Mwisho ya Ijumaa ya Ramadhani Msikiti wa Al-Aqsa iliuhudhuriwa na waumini 250,000

23:35 - April 15, 2023
Habari ID: 3476874
TEHRAN (IQNA) – Waislamu wapatao 250,000 wa Kipalestina walishiriki katika Sala ya mwisho ya Ijumaa ya Ramadhani 2023 katika Msikiti wa Al-Aqsa jana.

Zaidi ya polisi 3,200 wa utawala wa katili wa Israel, polisi wa mpakani na vyombo vya usalama vya Shin Bet waliwekwa kwenye barabara zinazoelekea msikitini katika mji mtakatifu wa al-Quds (Jerusalem)

Ramadhani ni nafasi adimu kwa Wapalestina wengi kutembelea al-Quds na kuswali Al-Aqsa. Kwa wengi, hii ilikuwa mara yao ya kwanza katika jiji hilo.

Ahmed Khassib, 51, kutoka Ramallah, amesema: "Nina furaha kuweza kuswali sala ya nne ya Ijumaa ya Ramadhani katika Msikiti wa Al-Aqsa.

"Siwezi kupata kibali cha kuswali katika Msikiti wa Al-Aqsa isipokuwa Ijumaa wakati wa Ramadhani, kwa hivyo nasubiri fursa hii mwaka mzima."

Akiswali msikitini, Khasib alisema kuswali hapo, "hubeba ujumbe kwamba Al-Aqsa ni ya Waislamu."

Wakati wa khutba yake ya Ijumaa, Sheikh Ekrimeh Sabri, Imamu wa Msikiti wa Al-Aqsa, aliwaambia waumini: “Nyinyi mliokuja kwenye Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa kutoka sehemu zote za Palestina tukufu, ninyi ambao mmevuka vizuizi vya kijeshi visivyo vya haki, kufika al Aqsa iliyobarikiwa kwa swala ya Ishaa na sala ya Tarawehe ni kuwakumbusha Waislamu bilioni 2 wa ulimwengu kuhusu kutekwa Al-Aqsa.”

Abd Al-Salam Abu Askar, Mpalestina kutoka Ukanda wa Gaza anayeishi Ramallah, alisema kwamba maoni ya uchochezi kuhusu Al-Aqsa ya waziri wa usalama wa taifa wa Israel Itamar Ben-Gvir yamewafanya Wapalestina kuazimia zaidi kupinga vikwazo vya Israel dhidi ya Al-Aqs na hivyo wamefika hapo kwa ajili ya ibada.

3483212

captcha