IQNA

Zilzala Syria na Uturuki

Misaada ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Hussein AS yawafikia Wasyria waliokumbwa na Zilzala

14:08 - February 18, 2023
Habari ID: 3476580
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Hussein AS imetuma timu ya madaktari kaskazini mwa Syria kwa ajili ya kutoa misaada kwa wale walioathiriwa na mItetemeko mkubwa ardhi.

Timu hiyo ina wataalam 40 na madaktari. Kulingana na idara hiyo, baadhi ya wagonjwa wa Syria wataletwa Iraq kwa matibabu zaidi.

Mitetemeko miwili ya ardhi ilikumba eneo la kusini mwa Uturuki mnamo Februari 6, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa Uturuki na mikoa ya kaskazini mwa Syria.

Tetemeko la kwanza la  ardhi la ukubwa wa 7.8 katika kipimo cha Rishta lilitikisa kusini mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria Jumatatu asubuhi ya tarehe 6 Februari. Kitovu chake kilikuwa ni katika mji wa Gaziantep wa Uturuki ambapo mamia ya majengo yameporomoka.Masaa machache baadaye kulijiri mtetemeko mwingine wa ardhi uliokuwa na ukubwa 7.6 kwenye kipimo cha rishta. Baada ya hapo pia kumejiri idadi kubwa ya mitetemeko midogo.

Takriban watu 45,000 wamethibitishwa kufariki katika nchi zote mbili huku idadi ya vifo ikitarajiwa kuongezeka.

Wakati huo huo, vikwazo vya miaka mingi dhidi ya Syria ambavyo vimewekwa na Marekani na waitifaki wake vimetatiza uwasilishaji wa misaada kwa taifa hilo lililokumbwa na vita.

 

4122813

Kishikizo: syria uturuki zilzala
captcha