IQNA

Krismasi

Rais wa Iran katika ujumbe wa Krismasi: Isa bin Maryam alikuwa Mtume wa amani na ukarimu

19:47 - December 25, 2020
Habari ID: 3473489
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia salamu za pongezi viongozi wa dunia kwa mnasaba wa kukumbuka kuzaliwa Nabii Isa Masih-Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake- na kuwadia mwaka mpya wa 2021 Miladia.

Katika ujumbe wake huo, Rais Rouhani ameongeza kuwa leo dunia inakumbwa na migogoro ya kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa na hivyo kuna haja ya kuwepo ushirikiano  wa viongozi wa nchi mbali mbali ili kujikwamua kutoka katika migogoro hii. Rais wa Iran amesisitiza kuhusu ushirikiano zaidi katika kukabiliana na kirusi cha corona ili maisha yarejee katika hali ya kawaida.

Rais Rouhani ameendelea kusema kuwa Nabii Isa bin Maryam-Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-alikuwa mtume wa amani na maelewano na mbebe bendera ya ukarimu. Ameelezea matumani yake kuwa, mwanadamu wa leo, hasa wafuasi wa Mitume wa Mwenyezi Mungu watafuata mafundisho ya mitume  ili mwanadamu aweze kufikia ubora.

Rais wa Iran amewatakia viongozi wa dunia afya, salama na mafanikio ya mataifa na serikali zao.

3943155

captcha