IQNA

Njama ya kumuua Sayyed Hassan Nasrallah

16:16 - January 14, 2016
2
Habari ID: 3470043
Kumefichuliwa njama ya pamoja ya nchi kadhaa ya kutaka kumuua Sayyid Hassan Nasrallah, katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
Njama ya kumuua Sayyed Hassan Nasrallah

Kwa mujibu wa gazeti la Al Diyar la Lebanon, Jawad Nasrallah ,mwana wa kiume Sayyid Hassan Nasrallah amefichua mpango huo hivi karibuni.

Kwa mujibu wa mkanda wa video uliofichuka, kunatekelezwa njama ya kumuua Sayyid Nasrallah na kwamba njama hiyo inapangwa na mashirika ya kijasusi ya Saudi Arabia, Bahrain na ba baadhi ya nchi za Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi zilivoshirikiana na mashirika ya kijasusi ya Mossad ya Israel na CIA ya Marekani.

Mzungumzaji katika mkanda huo wa video anasikika akisema kufuatia hotuba ya Sayyid Hassan Nasrallah baada kuuawa shahidi Sheikh Nimr, baadhi ya watawala wa eneo walikasirika na kughadhabika sana. Kwa msingi huo Shirika la Kijasusi la Saudia lilipokea amri kutoka kwa Mfalme wa Saudia kumuua Sayyid Nasrallah na kwamba jina la kiongozi huyo wa Hizbullah liwe katika orodha ya watu wanaopaswa kuuawa mara moja.

Katibu Mkuu wa Hizbullah manmo tarehe 3 Januari katika hotuba kwa njia ya televisheni alisema: "Kuawa Sheikh Nimr Baqir al Nimr , zaidi ya wakati wowote ule, kumeweka wazi kwa walimwengu uso wa utendaji jinai na ukufurishaji wa mfumo unaotawala Saudia."

Aidha Sayyid Nasrallah aliashiria njama na uwekezaji wa Saudia katika kuibua mifarakano katika ulimwengu wa Kiislamu na kusema: " Utawala wa Saudia unahusika katika kila sehemu panapo shuhudiwa mizozo baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni."

Katibu Mkuu wa Hizbullah pia katika hotuba yake hiyo ambayo iliwakera sana watawala wa ukoo wa Aal Saud alibainisha kuwa: "Vitabu ya shule Saudia ndio vitabu ambavyo pia vinatumiwa katika shule za kundi la kigaidi la Daesh (ISIS).

3467434

Imechapishwa: 2
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
abuuraahim
0
0
Assalaam aleikum. Ivi Saudi hakikA yake. Haswa nI nani.. yaani yeye nI aali. Saudi au aali. Yahudi? Kwa. HakikA muislamu. Kamili. Hawi ktk kuwafarakanisha waislamu kama Ivi.
Mohamed Farooque.
0
0
Nana ya kumuua Sayyid Hassan Nasrallah no dalili ya uoga walionao watawala wa Saudia. Hata wakifanikiwa, watakua wamefanya kazi ya bure maana Nasrallah wengine wako. Hawataweza kuizima Hizbollah wao ndio watakaoangamia. Muda wao ulobakia mfupi sana. Mwenyezi Mungu amhifadhi Sayyid H. Nasrallah.
captcha