IQNA

Turathi za Kiislamu

Msikiti Mkuu wa Kilwa nchini Tanzania, turathi ya kihistoria

17:56 - August 15, 2023
Habari ID: 3477439
KILWA (IQNA)- Msikiti Mkuu wa Kilwa Ni msikiti mkongwe sana katika kisiwa cha Kilwa Kisiwani, katika Mkoa wa Lindi nchini Tanzania.

Aghalabu ya nyaraka za kihistoria zinaonyesha kuwa ulijengwa katika karne ya kumi, lakini hatua kuu mbili za ujenzi ni za karne ya kumi na moja au kumi na mbili na kumi na kwa mtiririko huu. Ni miongoni mwa misikiti ya mwanzo iliyosalia katika mwambao wa Afrika Mashariki na ni miongoni mwa misikiti ya kwanza kujengwa bila ua.

Katika msikiti huu, ambao sasa hautumiki tena na kilichobakia ni magofu, kuna ukumbi mdogo wa Sala wa kaskazini ambao ulikuwa awamu ya kwanza ya ujenzi na ulijengwa katika karne ya 11 au 12.

Msikiti huu ulikuwa na nguzo tisa, ambazo awali zilichongwa kutoka kwa matumbawe lakini baadaye zikabadilishwa na mbao. Muundo huu, ambao ulikuwa umeezekwa paa, lulikuwa mmoja wa misikiti ya kwanza kujengwa bila ua.

Inadokezwa kuwa msikiti huu ulikarabatiwa katika karne ya 13.

Kwa mujibu wa wataalamu wa historia, kabla ya Kilwa Kisiwani kutawaliwa na wageni kutoka nchi za mbali, kilikuwa kinakaliwa na jamii za Waswahili na kiongozi anayetambulika kwa jina la Mndimbo katika karne ya saba.

Hata hivyo, anasema baada ya hapo wageni kutoka nchi za Uarabuni walianza kufurika katika kisiwa hicho.

Mwanaikolojia Dk Neville Chittick aliyefanya utafiti wake kuanzia mwaka 1955 akifukua udongo uliokuwa umefunika utajiri wa historia ya visiwa hivyo.

Anasema awali visiwa hivi vilikuwa ni vya Waswahili wakiongozwa na kiongozi wao ajulikanaye kama Mzee Mndimbo. Baadaye walikuja Washirazi na utawala wao wa kisultani.

Inaarifiwa kuwa Kilwa ilikuwa mji mkubwa kuanzia mwaka 1000 Miladia wakati majengo ya mawe yalipoanza kujengwa yakienea eneo la umbali wa kilometa moja ya mraba.

Kilwa ilikuja kuwa kituo kikubwa cha biashara kuanzia mwaka 1,100 hadi 1,500 Miladia ikiwa chini ya Sultan wa Shirazi, Ali ibn al-Hassan.

Baadhi ya watu mashuhuri waliotembelea Kilwa  ni pamoja na mfanyabiashara kutoka Morocco, Ibn Batuta aliyefika mwaka 1331 Miladia.

Mnamo 2005 na 2009, mradi uitwao Zamani Project, ambao ulizinduliwa nchini Afrika Kusini kuweka kumbukumbu za urithi wa kitamaduni wa Kiafrika, uliweka baadhi ya magofu ya Kilwa ikiwa ni pamoja na Msikiti Mkuu katika muudo katika 3D.

 

 

4162094

Kishikizo: kilwa washirazi
captcha