IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Israel inadhoofika, nguvu ya kujihami wanamapambano wa Palestina iimarishwe

22:42 - May 12, 2023
Habari ID: 3476990
TEHRAN (IQNA)-Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameeleza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umepoteza uwezo wake na kusema: Nguvu ya kujihami ya kambi ya muqawama inapasa kuimarishwa, na muqawama wa Palestina unapaswa kuendeleza njia hiyo kwa nguvu na fahari.

Katika hotuba za Sala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran, Hujjatul-Islam Walmuslimin Mohammed Javad Haj Ali Akbari amegusia matukio ya hivi sasa huko Palestina na kusema: Katika hotuba yake ya Idul Fitr, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema kwamba stratijia ya Ulimwengu wa Kiislamu hii leo inapaswa kuwa kusaidia wapiganaji wa ndani ya Palestina, na stratijia hii imepiga hatua katika njia iliyoainishwa kutoka kwenye Intifadha ya Mawe hadi Intifadha ya Makombora kwa himaya na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kuzifanya siku za utawala ghasibu wa Israel kuwa usiku za giza totoro. 

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa, Wazayuni wanakabiliwa na hali mbaya sana na kuongeza kuwa: Utawala huo unaoelekea kusambaratika, umekimbilia kwa mmoja kati ya wanasiasa katili zaidi ili kuunda baraza la mawaziri kwa ajili ya kujinusuru, lakini serikali hiyo ya wahalifu haikuweza kufanya chochote, na kinyume chake, hali imezidi kuwa mbaya.

Hujjatul-Islam Walmuslimin Haj Ali Akbari ameashiria jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni za kuwaua shahidi watu wasio na hatia wa Palestina na kusema: Mauaji ya watoto yanayofanywa na Israel yanaonyesha kukata tamaa na kufilisika kwa utawala huo.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesisitiza kuwa, mataifa yote ya Kiislamu yanapaswa kuunga mkono muqawama na mapambano ya ukombozi ya Palestina ili waweze kufikia hatua ya kujihami. Ameongeza kuwa: Katika hali ya hivi sasa, ni wajibu wetu sote kuunga mkono muqawama wa Palestina.

Wapalestina wasiopungua 30 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 90 kujeruhiwa katika mashambulizi ya kinyama yanayoendela kufanywa na utawala katili wa Israel dhidi maeneo ya Ukanda wa Gaza. 

414038

captcha