IQNA

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kwa mataifa yanayozungumza Kihispania

Mataifa yanayopigania haki na uadilifu yazidi kujuana na kushirikiana

17:46 - March 11, 2023
Habari ID: 3476691
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika salamu zake kwa mataifa yanayozungumza Kihispania juu ya kuzidi kujuana na kushirikiana mataifa yanayotetea haki na uadilifu.
Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Ofisi ya Hifadhi na Uchapishaji Athari za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, salamu za Ayatullah Khamenei kwa mataifa yanayozungumza Kihispania zimefikishwa sambamba na kuzinduliwa toleo la Kihispania la kumbukumbu za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Caracas, Venezuela.
Katika salamu na ujumbe wake huo wa maandishi Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesema: "itakuwa ni furaha kubwa sana kwangu kama nitakuwa nimeweza kuwasiliana nanyi wazungumzaji wa Kihispania kupitia kitabu hiki".
Ayatullah Khamenei ameongezea kwa kusema: "Hii ni sehemu fupi ya historia yangu. Ni uzuri ulioje kama sisi na nyinyi pamoja na mataifa yote yanayotetea haki na uadilifu tukazidi kujuana na kushirikiana. Namuomba Mungu akupeni bahati njema".

Uzinduzi wa toleo la Kihispania la kumbukumbu za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu yenye jina la "Seli Nambari 14" umefanyika katika hafla maalumu huko Caracas, mji mkuu wa Venezuela, sambamba na maonyesho ya utamaduni ya Urafiki wa Iran na Venezuela, yaliyoandaliwa kwa hima ya wanaharakati wa kitamaduni wa Venezuela na wazungumzaji wa Kihispania kwa kuhudhuriwa na shakhsia wa kiutamaduni wa Iran na Venezuela.

چه نیکوست که ما ملت‌های عدالت‌خواه با یکدیگر بیشتر آشنا شویم

Kitabu cha "Seli Nambari 14" kinasimulia kumbukumbu na wasifu wa Ayatullah Khamenei wakati wa mapambano dhidi ya utawala kibaraka wa mabeberu nchini Iran na kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

4127258

captcha