IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Twitter yasimamisha akaunti ya Qur’ani Tukufu yenye wafuasi Milioni 13

21:55 - February 06, 2023
Habari ID: 3476522
TEHRAN (IQNA) – Mtandao wa kijamii wa Twitter umetangaza kusimamisha kwa muda akaunti ya Qur'ani Tukufu ambayo ina wafuasi milioni 13 kutokana na kile wakuu wa mtandao huo wa kijamii walichokiita kuwa eti ni ukiukaji wa miongozo yake.

Akaunti hiyo, inayojulikana kama  Al-Mushaf, kwa kawaida husambaza aya za Quran Tukufu na ina idadi kubwa zaidi ya wafuasi kati ya akaunti za Qur’ani Tukufu  kwenye Twitter.

Hatua hiyo dhidi ya Al-Mushaf imeibua hasira miongoni mwa Waislamu wengi wanaoichukulia hatua hiyo kuwa ya kibaguzi.

Wanasema Twitter inapuuza kwa urahisi maudhui ya chuki,  vurugu na uasherati lakini inasitisha akaunti inayotuma aya za Qur’ani

Wanashangaa jinsi kutwiti aya za Quran kunaweza kukiuka miongozo ya Twitter.

Mtumiaji wa Twitter alisema mtandao huo wa kijamii una matatizo na Uislamu lakini hauna matatizo na wasiomumini Mungu Mmoja na uasherati.

 4120045

captcha