IQNA

Umoja wa Kiislamu

Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu lafanyika Tanzania

23:11 - January 09, 2023
Habari ID: 3476377
TEHRAN (IQNA) – Kongamano la siku moja limefanyika nchini Tanzania, likilenga kuimarisha na kukuza umoja katika Umma wa Kiislamu.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na tawi la Tanzania la Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa (SAW) na kituo cha kitamaduni cha Iran nchini Tanzania mnamo Januari 6, 2023, ilishirikisha wasomi wa madehehbu za Shia na Sunni kutoka Iran na Tanzania.

Waliohudhuria waliwasilisha makala ambazo ziliangazia mwingiliano kati ya wanazuoni wa ulimwengu wa Kiislamu, mustakabali wa ulimwengu wa Kiislamu, itikadi potovu ya ukufurishaji na kadhia ya Palestina.

Akizungumza na IQNA, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa (SAW) tawi la Tanzania, Hujjatul Islam Ali Taghavi, alisema kuwa tukio hilo lililenga kujadili haja ya kukuza umoja wa Kiislamu.

Kusaidia mwamko wa utamaduni na maarifa ya Kiislamu, kutetea utakatifu wa Qur'an Tukufu na Sunnah, kukuza ukaribu baina ya madhehebu za Kiislamu, na kuunda msimamo wa pamoja katika kukabiliana na propaganda za maadui dhidi ya Uislamu ni miongoni mwa mada zilizo jadiliwa katika kongamano hilo muhimu, Hujjatul Islam Taghavi aliongeza.

Halikadhalika amesema maadui wanajaribu kuzusha mifarakano miongoni mwa Waislamu ili kudumisha satwa yao ya kibeberu duniani.

Tanzania Hosts Int’l Conference on Islamic Unity

4112608

captcha