IQNA

Hujuma ya kigaidi

Jeshi la IRGC la Iran kufuatilia wanaovuruga usalama wa nchi

21:14 - October 30, 2022
Habari ID: 3476008
TEHRAN (IQNA)- Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametoa onyo kali kwa maadui, akisema kuwa vikosi vya Iran havina kikomo linapokuja suala la kulinda usalama wa nchi.

Brigedia Jenerali Alireza Tangsiri aliyasema hayo leo Jumapili alipokuwa akihutubia kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Wanamaji la IRGC akimaanisha wazi machafuko ya hivi karibuni kote Iran na shambulio la hivi karibuni la kigaidi lililolenga madhabahu takatifu kusini mwa nchi hiyo.

"Tutaharibu usalama yeyeote atakayejaribu kudhuru usalama wetu na tutaondoa tishio lolote kwa kufuatialia mzizi wake," Tangsiri alisema.

Akizungumzia shambulio la kigaidi katika mji wa kusini wa Shiraz ambalo lilisababisha waumini watu 15 kuuawa shahidi , alisema: "Adui alipogundua kuwa shinikizo lake la juu zaidi dhidi ya Iran limeshindwa, alianza kuua raia wetu wasio na hatia."

Waumini 15, akiwemo mwanamke na watoto wawili, waliuawa shahidi na wengine 40 kujeruhiwa baada ya gaidi aliyekuwa na silaha nzito kushambulia Haram Takatifu ya Shah Cheragh huko Shiraz, Mkoa wa Fars, Jumatano kabla ya sala ya jioni. Kundi la kigaidi la Daesh Takfiri limedai kuhusika na shambulio hilo.

Katika ujumbe wake siku ya Alhamisi, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei alisema wahusika wa jinai hiyo "ya kutisha" bila shaka watakabiliwa na adhabu.

Rais wa Iran Ebrahim Raeisi pia alisema Jumatano kwamba baada ya kubaini sababu kuu za uhalifu wa kutisha huko Shiraz vikosi vya usalama vitatoa jibu madhubuti waliopanga na kutekeleza jinai hiyo.

Naye Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesisitiza kuwa, kwa kujitokeza kwao vilivyo katika kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu; muda wote wananchi wa Iran wamekuwa wakiidhalilisha na kuifedhehesha Marekani na kuthibitisha kivitendo matamshi ya Imam Khomeini MA kuwa Marekani haiwezi kulifanyia taifa la Iran upuuzi wowote.

Brigedia Jenerali Hossein Salami amesema hayo katika maziko ya watu waliouawa kwenye shambulio la kigaidi la Haram Tukufu ya Shah Cheragh ya mjini Shiraz, kusini magharibi mwa Iran na kuongeza kuwa, Mapinduzi matukufu ya Kiislamu hayawezi kutetereshwa na vitimbakwiri wachache waliolaghaiwa na maadui. 

Shirika la habari la Iran Press limeripoti habari hiyo na kunukuu matamshi ya Kamanda Mkuu huyo wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC akisema kuwa, kujitokeza kwa wingi mno wananchi wa Shiraz katika maziko ya wahanga wa shambulio la kigaidi  la haram ya Shah Cheraqh ni ushahidi wa kufeli vibaya maadui wenye chuki kubwa mno na taifa la Iran.

Amesema, kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran waliopevuka kifikra na wenye muono wa mbali katika maziko hayo kumeshindilia msumari wa mwisho kenye jeneza la Marekani, Israel na maadui wengine woga na dhalili.

Kamanda Mkuu wa  Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) pia amesema, machafuko ya hivi karibuni ya nchini Iran yamechochewa na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kuwa, maadui hao wamehamaki kutokana na kushindwa vibaya na taifa la Iran katika kipindi cha miaka 43 iliyopita.

Pia amesema, Marekani mtenda jinai, utawala wa Kizayuni na ukoo wa Aal Saud wameona jinsi siasa zao chafu zinavyofelishwa na ushawishi na nguvu za kisiasa na kimaanawi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hata katika maeneo ya mbali na bila ya shaka wanajua kuwa hawawezi kukabiliana na taifa la Iran.

4095577

captcha