Infaq maana yake ni kutoa sadaka au kutoa sehemu ya mali ya mtu kwa wale wanaohitaji. "Birr" ni neno la Qur'ani Tukufu linalorejelea haki, uchamungu, uadilifu na kila tendo la utiifu kwa Mwenyezi Mungu. Pia ni cheo kikubwa ambacho kimeahidiwa kwa wale wanaofanya mambo mema. Kulingana na baadhi ya riwaya, msimamo huo nyakati fulani hufafanuliwa kuwa ule wa wanadamu wanaostahili zaidi mbele za Mungu; Ahl al-Bayt (SA) yaani watu wa nyumba ya Mtume Muhammad SAW wako katika kundi hili.
Swali ni hili, ni nani anastahili kufurahia nafasi hii?
“Kabisa hamtafikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda. Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua." (Qur'ani Tukufu, Sura Al Imran, aya ya 92)
Kwa mujibu wa aya hii, mojawapo ya masharti ya kupata nafasi ya watu wema ni kutoa na kutoa sehemu ya mali anayoipenda mtu.
Allamah Tabatabai, mfasiri maarufu wa Qur'ani Tukufu aliyeandika Tafsi al Mizan, anamini kwamba mwanadamu anapenda kujilimbikizia mali kana kwamba hii ni sehemu ya maisha yake; upendo huu ni kwa kiasi kwamba ikiwa atapoteza sehemu ya mali aanahisi kuwa sehemu ya maisha yake imeharibiwa. Hii inaashiria umuhimu wa infaq kutoka kwa kile mtu anachokipenda kweli na akifanya hivyo hupelekea kufika kwenye nafasi ya “Birr”.
Wakati huo huo, mfasiri wa zama hizi wa Qur'ani Sheikh Mohsen Qara’ati ambaye ameandika Tafsir Nur anarejelea nukta 12 kuhusu aya hii: