Wizara ya Sheria ya Marekani ilitangaza hayo Ijumaa.
Mnamo Agosti 23 maafisa wa mahakama walimshtaki Herman Leyvoune Wilson, 45, wa Albuquerque, kwa kujaribu kutoa msaada wa nyenzo kwa kundi la kigaidi la Daesh kwa kuanzisha kituo cha Daesh huko New Mexico.
Kituo hicho kililenga kufundisha itikadi za Daesh, kutoa mafunzo ya "karate," na kuwa kambi kwa watu binafsi wanaojiandaa kupigana kwa niaba ya kundi hilo nchini Marekani na nje ya nchi, ilisema taarifa hiyo.
Wilson, anayejulikana pia kama Bilal Mu'Min Abdullah, alisaidia kuendesha jukwaa la mtandaoni ambalo lilipigia debe uandikishaji wa wanaotaka kujiunga na Daesh na kujadili mashambulizi nchini Marekani na nje ya nchi, ilisema taarifa hiyo.
Wanaume wawili waliohukumiwa mwezi Julai kwa kutoa msaada kwa Daesh walisema Wilson aliwaleta kwenye kundi hilo, waendesha mashtaka walisema.
Kristopher Matthews, 36, wa South Carolina na Jaylyn Molina, 24, wa Texas walisema Wilson aliwabadilishia na kuwafanya wafuate "itikadi za ISIS," taarifa hiyo ilisema.
Kwingineko, Awais Chudhary, 22, wa New York siku ya Ijumaa alikiri hatia ya kupanga shambulio la kisu katika mtaa wa Queens kwa niaba ya Daesh, Idara ya Sheria ilisema katika taarifa.
Daesh ni kundi la magaidi wakufurishaji na weledi wa mambo wanasema kundi hilo lilianzishwa kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja na Marekani kwa ushirikiano na waitifake wake hasa utawala haramu wa Israel kwa lengo la kueneza ghasia katika eneo la Asia Magharibi.
3480227