IQNA

Fikra za Imam Khoemini

Raisi: Imam Khomeini MA aliwatetea waliodhulumiwa na waliodhoofishwa katika ardhi

13:59 - June 04, 2022
Habari ID: 3475333
TEHRAN (IQNA)- Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ijumaa usiku alihutubu katika hafla ya mkesha wa mwaka wa 33 tokea alipoaga dunia Imam Khomeini (MA) muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliyofanyika katika Haram Takatifu ya mtukufu huyo na kusema: "Mapambano dhidi ya uistikbari na udhalimu ni kati ya maudhui asili za Fikra za Imam Khomeini MA."

Rais Raisi aliongeza kuwa: "Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Iran iligeuka na kuwa kimbilio la watu wanaodhulumiwa duniani.."

Leo 14 Khordad kwa mujibu wa Kalenda ya Hijria Shamsia sawa na tarehe 4 Mfunguo Pili Dhul-Qaadah mwaka 1443 Hijria, mwafaka na tarehe 4 Juni 2022 Miladia ni siku ya kukumbuka kuaga daunia Imam Khomeini -Mwenyezi Mungu Amrehemu- Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran Press, katika hotuba yake, Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwaokoa waliodhulumiwa  na waliodhoofishwa katika ardhi ni moja ya nukta muhimu sana katika fikra za kisiasa za Imam Khomeini (MA). Aliongeza kuwa watu wote waliodhulumiwa duniani walimtazama Imam kama kiongozi wao.

Akiendelea na hotuba yake, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliashiria kauli ya Imam Khomeini MA aliposema: 'Marekani haina ubavu wa kufanya chochote' na kuongeza kuwa, leo tunashuhudia msemaji wa Ikulu ya White House akitangaza wazi kuwa mashinikizo ya juu kabisa ya Marekani dhidi ya Iran yamefeli.

Raisi ameendelea kwa kubaini kuwa wanasiasa duniani ni wengi lakini siasa bila kumcha Mwenyezi Mungu huibua msiba kwa mwanadamu na kuongeza kuwa, siasa bila umaanawi ndio sababu ya Wapalestina kudhulumiwa kwa zaidi ya miaka 70 na pia ni chanzo cha kushuhudiwa mashindano ya silaha za atomiki duniani.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, mustakabli wa Iran ni mwema na uliojaa nuru na kuongeza kuwa: "Nukta hii inapatikana katika miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Imam Khomeini MA."

3479165

captcha