IQNA

Itikafu yaruhusiwa tena katika Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina

22:37 - March 23, 2022
Habari ID: 3475070
TEHRAN (IQNA)- Wakuu wa Saudi Arabia wameruhusi tena ibada ya Itikafu katika Misikiti Miwili Mitakatifu ambayo ni Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al Masjid Al Haram, na halikadhalika katika Msikiti Mtakatifu wa Mtume SAW, Masjid an-Nabawi, mjini Madina.

Itikafu itaanza tena katika kipindi cha siku chache zijazo wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya kusimamishwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na janga la corona.

Tangazo hilo limetolewa na mkuu wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu  Dkt. Abdul Rahman Sudai ambaye amesema taratibu za kufuatwa na wanaoshiriki Itikafu zitatangazwa hivi karibuni.

Kabla ya kuzuiwa kwa muda, karibu waumini laki moja walikuwa wakishriki katika Itikafu katika misikiti hiyo miwili wakati wa siku 10 za mwisho za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Hivi kairbuni pia mijumuiko mkiubwa ya futari itaruhusiwa tena katika Misikiti Miwili Mitakatifu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani baada ya kuzuiwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na janga la COVID-19.

Haya yanakuja siku chache baada ya  uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi kuondoa kanuni zilizokuwa zinatakelezwa za kuzuia kuenea corona zikiwemo za kutokaribiana waumini  Msikiti Mkuu wa Makkah, Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina na misikiti mingine. Aidha si sharti tena waumini kuvaa barakoa.

Aidha si sharti tena kwa waumini wanaoenda Saudia kwa ajili ya Hija Ndogo au Umrah kuwa na chanjo ya corona au vipimo vya corona.

3478259

captcha