IQNA

Msikiti mpya wafunguliwa Lusaka, Zambia

21:57 - November 06, 2021
Habari ID: 3474525
TEHRAN (IQNA)- Msikiti mpya umefunguliwa hivi karibuni katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka kwa lengo la kuwahudumia Waislamu na pia kuelimisha watu wa nchi hiyo kwa ujumla kuhusu Uislamu.

Kwa mujibu wa taarifa msikiti huo wenye ukubwa wa mita mraba 7,000 umejengwa kwa kutegemea misaada ya Waislamu wa zamani.

Sherehe za kufungua msikiti huo zimehudhuriwa na wageni akdhaa rasmi akiwemo mhubiri na msomo wa Kiislamu mwenye asili ya Lebanon ambaye ameishi miaka mingi barania Afrika Sayyid Murtadha Murtadha, Mufti Mkuu wa Zambia Sheikh Asadullah Mwale na  Sayyid Muhsin Musavizadeh, mwakilishi wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu nchini Zambia.

Msikiti huo unalenga pia kuwa na kituo cha Kiislamu, ukumbi wa kidini ujulikanao kama Hussainiya na pia kitengo cha elimu.

 

 

 
 
 

3476357

Kishikizo: zambia msikiti waislamu
captcha