IQNA

Jiunge na Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran kwa kuwasilisha qiraa yako + Video

15:38 - March 10, 2021
Habari ID: 3473723
TEHRAN (IQNA) – Usiku wa Jumanne ulikuwa wa nne katika fainali za mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran.

Katika usiku huu washiriki waliosalia katika kitengo cha qiraa waliweza kusoma ambapo jopo la majaji lilitathmini qiraa hizo.

Washiriki katika kikao cha jana walikuwa ni kutoka Indonesia, Lebanon, Iraq, Egypt, Iran, Syria na Afghanistan ambapo walishiriki kwa njia ya intaneti kutokana na janga la corona.

Hivi sasa unaweza ukasikiliza klipu zilizo hapa chini za qiraa katika mashindano haya ya 37 ya kimataifa ya Qur'ani,  na kisha uige sauti uipendayo katika qiraa hizo na baada ya kujirekodi  tuma katika anuani ya @iqnanewsadmin  kabla ya Machi 18.

Qiraa yako ya Qur'ani tukufu itawekwa katika tovuti ya IQNA na washindi watatangazwa Aprili 18.

 

Join Iran Int’l Quran Competition by Submitting Your Recitations  

 

3958668/

captcha