IQNA

Msikiti wahujumiwa kwa mawe Ujerumani

14:53 - May 09, 2020
Habari ID: 3472750
TEHRAN (IQNA)- Watu wasiojulikana wameushambulia kwa mawe msikiti katika mji wa Cologne nchini Ujerumani katika tukio la chuki dhidi ya Uislamu.

Kwa mujibu wa taarifa, hujuma hiyo imeulenga Msikiti wa Chorweiler na hapakuwa na uharibifu mkubwa.  Taswira za video za usalama (CCTV) zimeonyesha watu wawili wakirusha mawe katika milango ya msikiti huo  usiku wa kuamkia Jumamosi. Msikiti uliohujumiwa , sawa na misikiti mingine Ujerumani umefungwa kwa takribani wiki saba sasa katika hatua zilizochukuliwa kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Mwenyekiti wa Msikiti wa Chorweiler, İbrahim Altun, amesema wameripoti tukio hilo kwa Polisi ya Ujerumani na uchunguzi ungali unaendelea. Amesema  wametaka maafisa  wa usalama  wawakamte mara moja wahusika ili wafikishwe kizimbani.

Ujerumani imeshuhudia ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu na wahamiaji katika miaka ya hivi karibuni, chuki ambazo zinachochewa na vyama vya mrengo wa kulia vyenye misimamo ya kuvurutu ada dhidi ya watu wasiokuwa Wajerumani asili.

Ujerumani ni nchi yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 81 na ina Waislamu takribani milioni tano na hivyo kuifanya nchi ya pili kwa idadi ya Waislamu Ulaya Magharibi baada ya Ufaransa.

3897470

captcha