IQNA

Rais Assad: Erdogan anaunga mkono magaidi wa Kitakfiri

14:05 - March 05, 2015
Habari ID: 2930963
Rais Bashar al-Assad wa Syria amekosoa vikali hatua ya Uturuki ya kuyaunga mkono makundi ya kigaidi na kitakfiri na kubainisha kwamba, Rais wa nchi hiyo Raccep Tayyip Erdogan anayaunga mkono makundi ya kitakfiri kwa ajili ya kuhudumia mabwana zake.

Rais wa Syria amelaani vikali hatua ya Uturuki ya kuyaunga mkono makundi ya kigaidi na kitakfiri yanayopigana dhidi ya serikali ya Damascus. Akizungumza mjini Damascus na ujumbe wa vyama vya siasa na asasi za Uturuki unaoundwa na shakhsia wa kisiasa, kiuchumi na viongozi wa vyama vya kisiasa, Rais Bashar al-Assad amesisitiza kuwa, ugaidi hauwezi kutokomezwa kwa vita na mapambano tu bali madola yanayowaunga mkono magaidi yanapaswa kusitisha himaya na uugaji mkono wao. Amesema, wananchi wanapaswa kuzishinikiza serikali zao ili ziache kuunga mkono ugaidi. Ujumbe huo umesisitiza katika mazungumzo yake na Rais Bashar al-Assad kwamba, akthari ya wananchi wa Uturuki wanafungamana na uhusiano wa kirafiki kati ya Damascus na Ankara na wanapinga hatua ya Rais Erdogan ya kuyaunga mkono makundi ya kigaidi.../mh

2925716

captcha