IQNA

Tarjuma Mpya ya Qur'ani kwa lugha ya Kiswahili

10:48 - January 16, 2013
Habari ID: 2481198
Taasisi ya Al Itrah ya Tanzania imechapisha tarjuma mpya ya Qur'ani kwa lugha ya Kiswahili. Kwa mujibu wa tovuti ya alitrah.info tarjuma hiyo imetayarishwa na Shaikh Hassan Ali Mwalupa, msomi maarufu wa Qur'ani Afrika Mashariki na kuhaririwa na Abdallah Mohammad. ya Al Itrah ya Tanzania imechapisha tarjuma mpya ya Qur'ani kwa lugha ya Kiswahili.
Taasisi ya Al Itrah yenye makao yake katika mji wa Dar es Salaam Tanzania imesema tarjuma hii ilichapishwa kwa mara ya kwanza Machi 2012 na kwamba chapa ya kwanza ina nakala 10,000

Katika taarifa, mchapishaji amesema kuwa tafsiri hii itawawezesha wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kuifahamu na kuielewa Qur'ani vizuri zaidi kwa lugha yao.

Mpangilio wa tarjuma hii ni ule wa Kiarabu upande moja wa kurasa na tarjuma ya Kiswahili upande mwingine aya kwa aya.

Sheikh Hassan Mwalupa pia ametarjumi kikamilifu Tafsiri ya Qurani ya Al Kashif ya Allamah Muhammad Jawad Mughniya ambayo imetolewa juzuu moja moja.

Katika utangulizi, mtarjumi Sheikh Hassan Mwalupa amesema ni matumaini yake kuwa wasomaji watafaidika na kazi hii na kuendelea kuunga mkono juhudi za Qur'ani kwa dua, masahihisho na mengineyo.

1172096
captcha