IQNA – Shirika moja la utetezi wa haki limeshutumu agizo jipya kutoka kwa serikali ya Trump linalozuia utoaji wa misaada ya majanga kwa majimbo na miji ya Marekani inayopinga bidhaa na makampuni ya Israel yanayoshiriki katika uhalifu wa kivita, likilitaja kuwa si la kizalendo, linakiuka katiba, na ni shambulio dhidi ya haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.
IQNA – Jenan Nabil Mohammed Nofal ni hafidha wa Qur’ani Tukufu anayewakilisha Palestina katika Mashindano ya 65 ya Kimataifa ya Usomaji na Uhifadhi wa Qur’ani yanayofanyika nchini Malaysia.
IQNA – Mashindano ya tatu ya kila mwaka ya kuhifadhi Qur’ani yanayoandaliwa na Msikiti Mkuu wa Al-Azhar nchini Misri yatafanyika kwa ushirikiano na benki ya Kiislamu.
IQNA – Wizara ya Wakfu na Mwongozo ya Yemen imetangaza kuwa itafanya mtihani maalum kwa ajili ya kuwachagua wawakilishi wa nchi hiyo watakaoshiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika mataifa mbalimbali.
IQNA – Kundi la kwanza la wahudumu wa Qur'ani kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, walioko katika Msafara wa Qur'ani wa Arbaeen, wamewasili Iraq mapema wiki hii na wameanza kufanya shughuli mbalimbali za Qur'ani katika mji mtukufu wa Najaf.
IQNA – Shirika la kutetea haki za Waislamu nchini Marekani limelaani vikali vifo vya raia wa Gaza vinavyosababishwa na njaa inayosababishwa kimakusudi na utawala wa Kizayuni wa Israel katika ukanda wa Palestina.
IQNA – Malaysia imezidisha juhudi za kuitangaza Qur'an Tukufu kama mwongozo wa maisha yenye maadili, kwa lengo la kulea kizazi chenye msingi imara wa tabia njema na uchamungu.
IQNA – Mohsen Qassemi, aliyeteuliwa kuiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani nchini Malaysia, alitoa qiraa’ yake Jumapili usiku katika ukumbi wa mashindano hayo mjini Kuala Lumpur.
IQNA – Mamlaka za Iraq zimezindua maandalizi makubwa ya huduma na usalama, huku mamilioni ya wafanyaziara wakitarajiwa kuelekea Karbala kwa ajili ya matembezi ya Arbaeen.
IQNA – Ofisi ya kiongozi mkuu wa Kishia nchini Iraq, Ayatullah Ali al-Sistani, imetoa tamko la kuzuia taasisi za kisiasa na za huduma kutumia picha yake katika maeneo ya wazi, hasa wakati wa hija ya Arbaeen inayokaribia.
IQNA – Mkurugenzi wa Msafara wa Hijja wa Iran ameifu mshikamano wa kimataifa uliodhihirika wakati wa vita vya siku kumi na mbili vilivyoanzishwa na utawala wa Israel dhidi ya Iran, na ametilia mkazo umuhimu wa umoja wa Waislamu kuelekea Siku ya Arbaeen ya Imam Hussein (AS).
IQNA – Mashindano ya 65 ya Kimataifa ya Usomaji na Kuhifadhi Qur’ani Tukufu (MTHQA) yamefunguliwa rasmi katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur, siku ya Jumamosi.
IQNA – Picha zilizopigwa mwishoni mwa Julai 2025 zinaonesha athari za mashambulizi ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya mji mkuu wa Iran, Tehran, mwezi Juni, ambapo maeneo ya makaazi ya raia yalilengwa.