IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Mashambulizi ya kigaidi dhidi ya misikiti yaongezeka Ujerumani

17:35 - August 10, 2023
Habari ID: 3477410
TEHRAN (IQNA)- Ongezeko la mashambulizi dhidi ya misikiti katika nchi za Magharibi hususan Ujerumani na barua za vitisho zinazotumwa kwa Waislamu vinazusha hofu na mfadhaiko katika jamii ya wafuasi wa dini hiyo.

 

Kutukana na kuvunjia heshima Uislamu na mambo matakatifu ya Kiislamu, kama Mtume (saw) na Qur'ani Tukufu, kwa kisingizio cha uhuru wa kusema, kumeruhusiwa katika nchi za Magharibi, ikiwemo Ujerumani, na serikali na sheria za nchi hizo zinawaunga mkono watu wanaopiga vita Uislamu wakiwemo watu wenye siasa kali za mrengo wa kulia.

Kwa sababu hiyo, mwelekeo wa chuki dhidi ya Uislamu na ukatili dhidi ya Waislamu umeongezeka katika nchi za Ulaya katika miaka ya hivi karibuni.

Kamal Ergon, Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya IGMG nchini Ujerumani, ametangaza kuwa mashambulizi dhidi ya misikiti nchini humo bado yanaongezeka, na kusema: Kazi ya kuwasaka wahusika wa mashambulizi kama yale ya kuchoma moto misikiti na taasisi za Kiislamu, ambayo yanaweza kugharimu maisha ya watu, inafanyika kwa mwendo wa kinyonga.

Burhan Kesici, Mkuu wa Baraza la Kiislamu la Ujerumani pia ametangaza kwamba, ongezeko la hivi karibuni la mashambulizi dhidi ya misikiti limesababisha hofu na mfadhaiko na kusema: "Tunatarajia mamlaka zitawalinda Waislamu."

Shirika la Kuzuia Uhalifu la Ujerumani limechapisha ripoti yake ya mwaka 2022 kuhusu idadi ya mashambulizi dhidi ya misikiti nchini humo, ambayo inaonyesha kuwa mashambulizi 62 ​​yalirekodiwa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 14 ikilinganishwa na mwaka 2021. 

3484721

Habari zinazohusiana
Kishikizo: ujerumani waislamu
captcha