IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Polisi Ujerumani wawapokonya Wazazi Waislamu mtoto kwa kupinga mafunzo potovu ya LGBTQ

13:09 - April 30, 2023
Habari ID: 3476935
TEHRAN (IQNA)-Filamu ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii imemuonyesha mtoto mdogo wa Kiislamu akiondolewa kwa nguvu katika familia yake ya Kiislamu na maafisa wa "huduma za ulinzi wa watoto" na askari polisi wa Ujerumani kwa sababu wazazi wake wanadaiwa kumfundisha kwamba mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja hayakubaliki katika Uislamu.

Video hiyo inawaonyesha jamaa wa familia hiyo waliojawa na hasira wakijaribu kuzuia kitendo hicho cha kikatili cha kunyang'anywa mtoto wao, huku mtoto mwenyewe akipiga mayowe na makelele kujaribu kujipapatua kutoka mikononi mwa maafisa wa polisi.

Mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii amelisimulia tukio hilo kwa kueleza kwamba, nchini Ujerumani, mtoto huenda shule, ambako hufunzwa mada ya 'ushoga', lakini mzazi wake anamwambia kuwa ni Haramu kulingana na dini yake. Kwa hivyo shule inawaita watu wa huduma za malezi ya watoto, na polisi hufika nyumbani na kumchukua kwa lazima kutoka kwa familia yake.

Mchangiaji mwingine ameandika: "hii imetokea Ujerumani na kuna kesi nyingi zinazofanana nayo katika nchi nyingi za Ulaya kama vile Sweden, ambako wanachukua watoto hao, sio tu kutoka familia za Kiislamu, lakini hata katika baadhi ya familia za Kikristo!" 

Tukio hilo la nchini Ujerumaini limejiri baada ya walimu wa mtoto huyo kujua kwamba wazazi wake walikuwa wakimfundisha kuwa ulawiti na usagaji ni dhambi kwa Waislamu. Walimu hao waliripoti kwa maafisa wa huduma za ulinzi wa watoto ambao waliwasiliana na polisi ili kwenda kumchukua mtoto huyo kwa nguvu nyumbani kwao.

Mnamo mwaka 2012, Kamati ya Nordic ya Haki za Kibinadamu (NHCR) ilimwandikia barua Katibu Mkuu wa Baraza la Ulaya kulaani vikali kile ilichokiita "uondoaji haribifu wa watoto" uinaofanyika katika nchi za Nordic ikiwemo Sweden.

"Familia nyingi za vijana, familia za mzazi mmoja, familia dhaifu kiuchumi na kielimu, familia zenye changamoto za kiafya na wazazi wahamiaji, wanalengwa na huduma za kijamii nchini Sweden, Norway, Denmark na Finland," barua hiyo ilisema.

Barua hiyo ya NHCR kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Ulaya ilibainisha pia kwamba, wazazi wenye imani za kidini na kifalsafa ambazo hazionekani kukubalika kisiasa, mara nyingi huchukuliwa kuwa ni wazazi wasiofaa, na hivyo kuyafanya Mabaraza ya Kijamii, yakishauriwa na wafanyakazi wa huduma za jamii, kuwaondoa watoto katika familia na makazi yao na kuwapeleka katika nyumba za kulea watoto.

3483362

captcha