IQNA

Mashindano ya Nne ya Qur'ani Ulaya kufanyika Ujerumani

13:04 - December 24, 2015
Habari ID: 3468966
Duru ya Nne ya Mashindano ya Kimataifa aya Qur'ani Barani Ulaya itfanyika nchini Ujerumaani kuanzia Machi 25-27 mwaka 2016.

Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Darul Qur'ani ya Ujerumani ambapo pia kutakuwa na washiriki wanawake na wanaume.
Kwa mujibu wa tovuti ya taasisi hiyo, mashindano hayo yatajumisha kategoria za qiraa, hifdhi, ufahamu wa Qur'ani na adhana.
Imearifiwa kuwa mashindano hayo yanalenga kuimarisha utamaduni na ufahamu wa mafundisho ya Qur'ani sambamba na kuimarisha vipawa vya Qur'ani na pia kuandaa jukwaa la kubadilishana mawazo na uzoefu kati ya wataalamu wa Qur'ani barani Ulaya.
Waislamu kutoka madhehebu zote za Kiislamu wanaoishi Ulaya wanakaribishwa kushiriki katika mashindano hayo.
Wale ambao wanakusudia kushiriki katika mashindano hayo wanapaswa kuarifishwa na vituo vya Qur'ani barani Ulaya au kutuma video au sauti ya qiraa yao kupitia barua pepe. Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea tovuti ya http://www.haus-des-koran.de/ au kupiga simu +494022948615 kutuma barua pepe au email kupitia news@izhamburg.com
Watakaoshika nafasi za awali watawakilisha bara Ulaya katika mashindano ya Qur'ani maeneo mengine duniani.


Kwa mujibu wa Shirika la Pew kuna Waislamu zaidi ya milioni 45 kote Ulaya ukiondoa Uturuki ambayo ni nchi ya Waislamu.

3468640

captcha