IQNA

Harakati za Qur'ani

Maelfu ya wafungwa wa Iran wahifadhi Qur’ani wakiwa gerezani

22:51 - April 26, 2024
Habari ID: 3478738
IQNA - Maelfu ya wafungwa katika jela za Jamhuri ya Kiislamu Iran wamefaulu kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu au juzuu kadhaa wakiwa wanatumikia vifungo vyao gerezani, mkuu wa Shirika la Magereza la Iran alisema.

Programu za Qur’ani Tukufu zinapewa kipaumbele katika  mipango ambayo inalenga kupunguza idadi ya wahalifu wanaorejea katika uhalifu, Gholamali Mohammadi aliiambia IQNA Jumatano.

Qur’ani Tukufu ni kitabu cha maisha na mwongozo, alisema na kuongeza kuwa vituo 518 vya Dar al-Quran vimeanzishwa katika magereza kote nchini Iran kwa ajili ya kuwaongoza wafungwa.

Afisa huyo amesema wafungwa wengi ambao hapo awali hawakuifahamu Qur’ani Tukufu, wamegundua mafundisho yake wakiwa gerezani, na kuongeza kuwa mtaala wa Qur'ani unashughulikia masomo ya kusoma, kuhifadhi na kufasiri.

Kutokana na programu hizi, idadi kubwa ya wafungwa wamefikia hatua za ajabu katika kuhifadhi Qur'ani, Mohammadi alisema, na kuongeza kuwa 1,517 wamehifadhi aya chache walizochagua, 2,362 wamehifadhi surah kamili, 482 wamehifadhi juzuu tatu, 252 wamehifadhi juzuu tano, 147 wamehifadhi. Juzuu 10, 75 wamehifadhi juzuu 15, 67 wamehifadhi juzuu 20, na 72 wamehifadhi Qur’an Tukufu kikamilifu..

Ili kuwahamasisha wafungwa kujifunza na kuhifadhi Qur’ani, ushiriki katika programu hizi unahusishwa na manufaa ya kisheria, alisisitiza afisa huyo. Baadhi ya wafungwa hata wameepuka adhabu ya kifo na wengine  kupata msamaha kupitia kujitolea kwao katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu, alisema.

Hadi sasa, mashindano matano ya Qur'ani yameandaliwa katika magereza, kimkoa na kikanda, alibainisha.

 4211814

captcha