IQNA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina

16:11 - September 03, 2020
Habari ID: 3473132
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa tena suala la kuanzishwa uhusiano baina ya Imarati na utawala ghasibu wa Israel na kusisitiza kuwa: Jambo lililofanywa na kawaida kwa uhusiano huo ni kubinya shingo la Wapalestina kwa goti la Wazayuni.

Katika ujumbe wake wa jana kwenye ukurasa wa mtandao wa Twitter Muhammad Javad Zarif alionesha picha ya askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel akigandamiza goti lake kwenye shingo la raia wa Palestina na kuandika kuwa: "Kuanzisha husiano wa kawaida na Israel? Kitu pekee kilichofanywa cha kawaida kwa uhusiano huu ni kubinya shingo la Wapalestina kwa goti la Wazayuni."

Hivi karibuni mitandao ya kijami ilionesha mkanda wa video wa askari mmoja wa Israel akimbinya shingo kwa goti raia wa Palestina aliyekamatwa katika maandamano ya amani huko Ukingo wa Magharibi.

Mwezi uliyopita Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza habari ya kufikiwa mapatano baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu na utawala haramu wa Israel kuhusu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya pande mbili. Hatua hiyo imelaaniwa na harakati zote za mapambano ya ukombozi wa Palestina na mataifa ya Kiislamu.  

3472453

captcha