IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Mbinu ya jadi ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika Kijiji cha Uhispania

21:50 - May 27, 2023
Habari ID: 3477055
TEHRAN (IQNA) - Waislamu katika kijiji cha Granada, mkoa wa kusini mwa Uhispania, wanajifunza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa kwa njia ya jadi. Kulingana na tovuti ya Tawasul, Kijiji cha Al-Kawthar katika mkoa wa Andalusia nchini Uhispania kina wakaazi 490.

Kijiji hicho kina idadi ya Waislamu wanaopenda kuhifadhi mila za Kiislamu. Wanavaa nguo za Kiislamu na kuwafundisha watoto wao kurusha mishale na kupanda farasi ikiwa ni katika kufuata Sunna ya Mtume Muhammad SAW.
Waislamu hao ambao wote wanatoka Granada, walinunua shamba kubwa na kuanzisha kijiji cha Al-Kawthar miaka michache iliyopita.
Kisha hujenga shule na msikiti ambamo watoto wao huhifadhi Qur'ani Tukufu kwa kutumia mbao za udongo.
Watu wengi waliokuja katika kijiji hiki pamoja na familia zao wamesoma sana na walikuwa na biashara katika sehemu nyingine za Uhispania lakini waliacha kazi zao na kuja hapa ili watoto wao wakue katika mazingira ya Kiislamu.
 
4143583

captcha