IQNA

Mwanamke mwenye umri wa miaka 69 ataraji kuhifadhi Qur'ani kikamilifu Uturuki

11:49 - April 08, 2017
Habari ID: 3470924
TEHRAN (IQNA)-Mwanamke raia wa Uturuki ambaye amehifadhi nusu ya Qur'ani hivi sasa anataraji kuhifadhi Qur'ani kikamilifu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Bi.Firuz Suntur ambaye anaishi katika mji wa Van mashairki mwa Uturuki alianza masomo ya Qur'ani hivi karibuni na si tu kuwa alifanikiwa kuweza kusoma kwa usahihi bali pia alihifadhi juzuu 15 za Qur'ani Tukufu.

Anasema kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuhifadhi Qur'ani kutokana na matatizo ya kimaisha na kukosa wakati. Anasema baada ya watoto wote kufanikiwa kuolewa sasa amepata muda wa kutosha kufanikisha lengo lake la muda mrefu.

Bi. Firuz anasema baadhi ya zamaa zake walikuwa wanaamini kuwa kwa umri wake hawezi kuhifadhi Qur'ani lakini anasema aliwapuuza na kusonga mbele na azma yake ya kuhifadhi Qur'ani.

"Nataraji kuwa siku moja nitaweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu," anasema.

Kwa hakika Bi. Firuzi ni thibitisho kuwa kwa nia na azma, mwanadamu anaweza kufikia malengo matukufu na mafanikio hayo hasa hupatikana kwa kutowasikiliza wenye kutoa matamshi yenye kuvunja moyo.

3587340
captcha