IQNA

Mashindano ya Qur’ani yafanyika Rwanda

22:59 - September 30, 2014
Habari ID: 1455972
Mashindano ya Qur’ani yamefanyika nchini Rwanda chini ya himya ya Jumuiya ya Waislamu nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi  Shirika la Kimataifa la Habari za Kiislamu (IINA), mashindano hayo yalikuwa na washiriki 50 wanawake na wanaume.
Mashindano hayo yamefanyika kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Mashindano hayo yalikuwa na kategoria kadhaa zikiwemo kuhifadhi Qur’ani kikamilifu, kuhifadhi Juzzu 20, 15,10, 5  na 2.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2006 , takribani asilimia 5 ya wakaazi wote milioni 11 nchini Rwanda ni Waislamu.
Jumuiya ya Waislamu wa Rwanda ilianzishwa mwaka 1964  kwa lengo la kuwakilisha Waislamu nchini humo sambamba na kueneza mafundisho ya dini ya Kiislamu na kutoa huduma za afya n.k.../mh

1455634

captcha