IQNA

Qur'ani Tukufu

Familia Bora ya Qur'ani Misri Yatangazwa

19:21 - December 25, 2023
Habari ID: 3478089
IQNA - Mshindi katika kitengo cha 'Familia ya Qur'ani' ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Misri ametangazwa

Duru ya 30 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu imeanza  katika Kituo cha Dar-ul-Quran cha Masjid Misr, cha mji mkuu mpya wa utawala wa Misri, Jumamosi, Disemba 23.

Katika siku ya pili ya tukio Jumapili, familia ya Mohammad Saad Issa ilitajwa kuwa mshindi katika kategoria ya Familia Bora ya Qur'ani, tovuti ya habari ya al-Misrawi iliripoti.

Familia hiyo itatunukiwa zawadi ya pesa taslimu pauni 500,000 za Misri.

Familia ya Mahmoud Ahmed Mahmoud Mukhlis ilikuwa mshindi wa pili, na kujishindia pauni 400,000.

Na familia ya Abdul Hamid Abdul Fattah Abuzuhra ilishika nafasi ya tatu, na kujishindia zawadi ya fedha taslimu pauni 300,000.

Wakati huo huo, mashindano yaliendelea katika kategoria nyingine chini ya usimamizi wa Sheikh Mohamed Hashad, rais wa Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani wa Misri.

Wawakilishi wa nchi 64 wanashiriki katika mashindano ya kimataifa, yaliyoandaliwa na Wizara ya Wakfu ya Misri.

Kulingana na Waziri wa Wakfu Sheikh Mohamed Mukhtar Gomaa, jumla ya zawadi za fedha taslimu kwa toleo hili zitakuwa zaidi ya pauni milioni 8 za Misri, ikiwa ni ukuaji wa asilimia 300 ikilinganishwa na toleo la mwaka jana.

4189713

captcha