Ali Barka, amenukuliwa na Televisheni ya Al Masirah kuwa taifa la Palestina linauawa kwa mabomu ya kisasa ya Marekani.
Ameeleza kuwa" "tumeingia katika kipindi cha mapambano makali na utawala wa Kizayuni unaelekea kwenye maangamizi na nchi zinazofanya mapatano nao zinapaswa kuangalia upya sera zao na kuongeza kuwa, makundi ya kupigania ukomboizi wa Palestina yatetea Msikiti wa Al-Aqsa na heshima ya taifa la Kiarabu.
Kiongozi huyo wa Hamas alitoa salamu kwa jeshi la Yemen lililoingilia kati kuunga mkono muqawama wa Palestina na kusema: "Wakati makombora na ndege zisizo na rubani zinarushwa kutoka Yemen, ina ujumbe kwamba Yemen kamwe haitaliacha taifa la Palestina peke yake."
Vile vile amesisitiza kuwa, adui Mzayuni anaelewa tu lugha ya mabavu na mapambano ya silaha au muqawama, na operesheni ya Kimbunga ya Al-Aqsa ilifungua mlango wa ukombozi (wa ardhi ya Palestina) na uwezekano wa kushindwa utawala wa Kizayuni umekuwa ukweli.
4179416