IQNA

Mmisri ashika nfasi ya pili ya mashindano ya Qur’ani ya Kazan, Russia

22:49 - May 29, 2022
Habari ID: 3475311
TEHRAN (IQNA)- Mahmoud Khaled Suwaid, mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Misri cha Al-Manofiyeh nchini, alishinda nafasi ya pili katika Mashindano ya Qur’ani yaliyofanyika mjini Kazan, nchini Russia.

Katika mahojiano na Televisheni ya Misri alisema: "Mashindano hayo yalifanyika kwa siku tatu katika mji wa Kazan (ambao ni mji mkuu wa Jamhuri ya Tatarstan katika  Shirikisho la Russia) Tatarstan), na washindi walitunukiwa zawadi siku ya nne.”

Aliongeza: "Mashidano yalikuwa magumu washiriki walikuwa na takribani kiwango kimoja na hatimay na mwakilishi wa Jamuri ya Chehenia akawa wa kwanza.”

Savid Suwaid: "Nilishiriki katika mashindano haya baada ya kuchaguliwa kwa majopo mawili ya Misri na umakini wangu mwingi katika mashindano hayo ulizingatiwa na majaji.”

Mwanafunzi huyo wa Misri alisema kuhusu shughuli zake za Qur’ani kwamba nilianza kuhifadhi Qur'ani katika shule yangu ya kijijini kutoka umri wa miaka mitatu na kabla ya kuwa na miaka 5, nilifanikiwa kuhifadhi Qur’ani Tukufukikamilifi.

Amesema pia ameshiriki katika mashindano kadhaa ya Qur’ani nchini Misri.

4060385

captcha