TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amesema kuwa, kushindwa na kufedheheka vitaukumba utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika vita yoyote ile itakayotokea, zaidi ya kushindwa kulikoukuta katika vita vya siku 33 vya mwaka 2006.
Sayyid Hassan Nasrallah aliyasema hayo jioni ya Jumapili ya jana mjini Beirut katika
sherehe za mwaka wa 11 wa ushindi wa harakati ya harakati ya Hizbullah
katika vita vya siku 33 mwaka 2006 kati ya harakati hiyo na utawala huo
wa ghasibu wa Kizayuni na kuongeza kuwa, siku kama ya jana ni siku kubwa
ambayo ndani yake wanamapambano wa Hizbullah walisimama imara na
kufelisha njama na juhudi za askari wa Israel za kutaka kuikalia kwa
mabavu ardhi ya Lebanon.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon
amefafanua kuwa, muqawama hauna haja ya kufikia stratijia za kisiasa
bali unafuatilia malengo makuu ya kitaifa na kwamba upande wowote
unaovizia kutaka kuona muqawama huo unashindwa, basi utashuhudia hasara
wenyewe, kama ambavyo pia upande wowote unaodhania kuwa mapambano (muqawama) ni
dhaifu, basi utaishia kushindwa. Sayyid Hassan Nasrallah amesisitiza
kuwa, wanamapambano shupavu wa muqawama katika vita ya siku 33 mwaka
2006 hawakuingia vitani kwa kutaka kujionyesha, bali kwa mapambano
halisi ambayo hata baada ya kupita miaka 11 tangu kujiri vita hiyo, adui
bado ameendea kuhisi fedheha na kukabiliwa na changamoto kubwa kutoka
kwa muqawama huo. Kiongozi huyo wa Harakati ya Hizbullah amebainisha
kwamba ugaidi, yaani Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel
unachora ramani juu ya maji ambayo itaishia kufeli. Sambamba na
kuashiria kuwa Marekani na Israel zinasema kuwa Hizbullah ina uwezo
mkubwa na hatarishi kwao, amesema kama ninavyomnukuu: "Ndio ni kweli
ina uwezo mkubwa, hususan juu ya njama za Israel."
Aidha Sayyid Hassan Nasrallah ameongeza kuwa, magaidi katika eneo
wameletwa na Wamagharibi kwa kushirikiana na washirika wao na hata Rais
Donald Trump katika kampeni zake za uchaguzi uliopita alikuwa
akisisitizia sana suala hilo na ameongeza kwa kusema, Marekani ndio
inayaunga mkono kifedha makundi ya kigaidi nchini Iraq na Syria na
kwamba, hata hivyo njama hizo hazitaweza kuidhoofisha harakati ya
Hizbullah ya Lebanon.
3463636