IQNA

Maulid ya Mtume Muhammad SAW

Waziri Mkuu wa Pakistan awataka Waislamu kusoma Sira ya Mtume Muhammad SAW

22:54 - September 28, 2022
Habari ID: 3475849
TEHRAN (IQNA) – Waziri Mkuu wa Pakistani ametuma salamu za kheri na pongezi kwa dunia nzima, hususan Umma wa Kiislamu, mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Rabi Al-Awwal.

Katika ujumbe wake wa Twitter siku ya Jumanne, Shehbaz Sharif pia alisema kwamba Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) ni chanzo cha mafanikio kwa wanadamu wote katika maisha dunia na kesho akhera.

Alilitaka taifa la Pakistani kuweka ahadi ya kusoma Sira ya Mtume Muhammad (SAW) katika mwezi huo na kuifanyia kazi ili wastahiki kupata shifaa ya Mtukufu Mtume SAW katika Siku ya Hukumu.

Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) alizaliwa katika Rabi Al-Awwal, mwezi wa tatu katika kalenda ya mwandamo ya Hijria Qamaria.

Kwa mujibu wa  Waislamu wa madhehebuya Shia, Mtume Muhammad (SAW) alizaliwa ya 17 ya Rabi al-Awwal huku Waislamu wa madhehebu ya Sunni wakiichukulia siku ya 12 ya mwezi huo kama siku ya kuzaliwa kwa mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu.

Kwa kuzingatia tarehe hizo mbili, Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu Amrehemu-alitangaza kuwa baina ya 12-17 Rabi al Awwal ni ‘Wiki ya Umoja wa Kiislamu’ ili kipindi hicho kiwe fursa ya kuleta mashikamano na maelewano miongoni mwa Waislamu duniani. 

3480658

captcha