IQNA

Rais wa Algeria asisitiza kuunga mkono Palestina

22:25 - June 08, 2021
Habari ID: 3473989
TEHRAN (IQNA)- Rais Abdelmajid Tebboune wa Algeria amesema nchi yake haitalegeza msimamo wake katika kuunga mkono taifa la Palestina.

Akizunguma na kanali ya televisheni ya Al Jazeera, amesema  hakuna mazingira yoyote ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mwaka jana Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na kisha Morocco zilianzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel. Nchi zingine za Kiarabu ambazo zimeanzisha uhusiano na utawala bandia wa Israel ni Jordan na Misri huku Saudi Arabia ikiripotiwa kuwa na uhusiano wa siri na utawala huo haramu.

Kitendo hicho cha nchi hizo  kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel ambacho ni sawa na kusaliti malengo ya Palestina kimekabiliwa na radiamali hasi katika Ulimwengu wa Kiislamu.

3474917

Kishikizo: algeria palestina israel
captcha