IQNA

Ayatullah Isa Qassim alaani 'bendera ya Mahusiano ya jinsia moja' katika ubalozi wa Marekani Bahrain

17:55 - June 07, 2021
Habari ID: 3473985
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Bahrain amejiunga na maulamaa nchini humo katika kulaani kitendo cha kupeperushwa bendera ya mahusiano ya jinsia moja katika ubalozi wa mji mkuu wa nchi hiyo, Manama.

Kwa mujibu wa taarifa, Ayatullah Sheikh Issa Qassim Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Bahrain ametuma ujumbe wa kulaani vikali kitendo cha ubalozi wa Marekani mjini Manama kupeperusha bendera ya kuunga mkono uhusiano wa jinsia moja. Sheikh Qassim amesema lengo la Marekani katika kupeperusha bendera hiyo ya ufuska ni kuhimiza vitendo ambavyo ni haramu kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

Sheikh Issa Qassim amesisitiza kuwa Bahrain ni Marekani na Wabahrain watapambana vikali na kitendo hicho cha Marekani.

Kwingineko, Muungano wa Vijana wa Harakati ya Februari 14 umetoa taarifa ukilaani vikali kitendo hicho, ambacho unasisitiza kuwa kinaenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu na thamani za kimaadili za taifa hilo.

Taarifa hiyo imeeleza bayana kuwa, hatua ya Marekani kupandisha bendera yenye nembo ya kuunga mkono usenge na usagaji katika jengo la ubalozi wake mjini Manama ni tusi kwa matukufu ya Kiislamu na kwa utamaduni wa watu wa Bahrain.

Muungano wa Vijana wa Harakati ya Februari 14 umebainisha katika taarifa hiyo kuwa, kitendo hicho cha Marekani hakina malengo mengine ghairi ya kushajiisha ufuska na mmomonyoko wa maadili katika taifa hilo dogo la Ghuba ya Uajemi.

Kadhalika taarifa hiyo imeukosoa vikali utawala Aal-Khalifa kwa kunyamazia kimya uchafu huo ambao si tu umehujumu mafundisho ya Uislamu, lakini pia umeumiza hisia za wananchi wa Bahrain.

Muungano wa Vijana wa Harakati ya Februari 14 umesisitiza kuwa, utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani na balozi mdogo wa US mjini Manama, Maggie Nardi wanapaswa kufahamu kuwa, wananchi wa Bahrain na vikosi vya kimapunduzi havitafumbia macho kitendo hicho cha kihaini na kichokozi, na vinataka kuheshimishwa mila, tamaduni na desturi za Wabahrain.

3976045

captcha