IQNA

Walowezi wa Kizayuni wauahujumu tena msikiti wa Al Aqsa

15:28 - June 03, 2021
Habari ID: 3473974
TEHRAN (IQNA)- Walowezi wa Kizayuni, wakiwa wanalindwa na askari wa jeshi la utawala haramu wa Israel Jumatano waliuhujumu na kuuvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa katiak mji wa Quds (Jerusalem).

Kwa mujibu wa taarifa Wazyauni hayo waliingia katika maeneo ya wazi ya msikiti huo na kutekeleza ibada za Kiyahudi huku wakidai kuwa eneo hilo linapaswa kujengwa kujengwa hekalu la Kiyahudi. Wapalestina waliokuwa hapo walikabiliana nao kwa amani huku wakitoa naraza la Allahu Akbar.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

3474878

captcha