IQNA

Vita vya Saudia dhidi ya Yemen

Wayemen walazimika kula majani ya msituni kutokana na njaa

21:42 - September 16, 2018
Habari ID: 3471675
TEHRAN (IQNA)- Idadi kubwa ya Wayemen sasa wanalazimika kula majani ya msituni kutokana na kusakamwa na baa la njaa ambalo limesababishwa na hujuma ya kivita ya Saudia dhidi ya nchi hiyo masikini zaidi ya Kiarabu.

Duru za habari zinadokeza kuwa, wakazi wa wilaya ya Aslam katika mkoa wa Hajjah, kaskazini magharibi mwa Yemen wamelazimika kula majani ambayo kawaida hayatumiki kama chakula ili kupunguza makali ya njaa inayowasakama.

Habari zinasema kuwa, akina mama katika maeneo hayo huchuma majani ya mti aina ya Halas au Wax kwa Kiingereza, na kuyaosha kabla ya kuyachemsha na kuyala.

Wayemen wanaokabiliwa na hujuma ya kijeshi ya Saudia wanalazimika kula majani  majani hayo ambayo huwa machachu sana na yenye asidi kali yakishachemshwa.

Hii ni katika hali ambayo, Mpango wa Chakula Duniani wa Umoja wa Mataifa (WFP) umetahadharisha katika taarifa yake juu ya mwenendo wa kuwafikishia misaada wananchi wa Yemen wanaokabiliwa na baa la njaa ambalo limesababishwa na mashambulio ya kijeshi na mzingiro wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia na kutoa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kukabiliana na hali hiyo.Wayemen walazimika kula majani ya msituni kutokana na njaa

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutoroka nchi. Hata hivyo Saudi Arabia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao hayo huku wakisababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasiopungua 15,000 wasio na hatia. Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa walipoteza maisha katika  vita dhidi ya Yemen vinavuyoongozwa na Saudia kwa himaya ya madola ya Magharibi hasa Marekani na utawala haramu wa Israel.

3466760

captcha