IQNA

Wanawake Waislamu wanaovaa Hijabu wanashambuliwa Ubelgiji

10:37 - September 10, 2018
Habari ID: 3471665
TEHRAN (IQNA)- Takwimu zinaonesha kuwa, asilimia 76 ya vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu nchini Ubelgiji mwaka 2017 vilihusu kushambuliwa wanawke Waislamu wanaovaa Hijabu.

Ripoti zinasema kuwa, Jumuiya ya Kimataifa ya Kuzuia Propaganda Chafu dhidi ya Uislamu nchini Ubelgiji (CCIB) imetoa ripoti kuhusu takwimu za mashambulizi yanayofanywa na makundi ya wanaopiga vita Uislamu mwaka 2017 na kutangaza kuwa, shambulizi moja la aina hiyo limekuwa likifanyika nchini Ubelgiji kila baada ya siku mbili.

Ripoti hiyo imesisitiza kuwa, karibu asilimia 29 ya mashambulizi hayo yamefanyika katika mitandao ya kijamii, 17 dhidi ya misikiti na vituo vya masomo vya Waislamu, asilimia 14 dhidi ya maeneo yao ya kazi na asilimia iliyokabia ya mashambulizi hayo yamefanyika dhidi ya wanawake wa Kiislamu katika maeneo mengine nchini humo. Halikadhalika ripoti hiyo imebaini kuwa wanawke Waislamu ndio wanaolengwa zaidi kutokana na kuwa ni rahisi kutmabua imani yao na idadi kubwa ya wanaowahujumu ni wanaume.

Mashambulizi na chuki dhidi ya Uislamu vimeenea sana barani Ulaya katika miaka ya hivi karibuni na vimeshika kasi kubwa zaidi katika nchi za katikati mwa bara hilo ikiwemo nchi ya Ubelgiji kutokana na kuibuka vyama vingi vya kibaguzi na vya mrengo wa kulia wenye kufurutu ada.

/3745163

captcha