IQNA

Wanafunzi wa shule karibu milioni moja Iran wamehifadhi Qur’ani

10:32 - June 20, 2018
Habari ID: 3471566
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Elimu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa karibu wanafunzi milioni moja nchini wamehifadhi Qur’ani.

Bw. Mikaeel Bagheri, Naibu Waziri wa Elimu Iran anayesimamua masuala ya Qur’ani , Swala na Etrat amesema kuna wanafunzi 950,000 waliohifadhi Qur’ani Tukufu nchini Iran.

Amesema wanafunzi hao wamehifadhi kuanzia nusu juzuu ya Qur’ani Tukufu hadi Qur’ani kamili.

Afisa huyo wa wizara ya elimu amesema wanafunzi milioni 4.5 walishiriki katika mashindano kadhaa ya Qur’ani, Swala na Etrat nchini Iran baina ya Machi 2017 na Machi 2018.

Halikadhalika amesisitiza umuhimu wa kutumia mbinu mpya, za kisasa na sahihi katika kuwafunza wanafunzi Qur’ani Tukufu na ufahamu wa aya za kitabu hicho kitukufu.

Kufuatia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979, nchi hii imepiga hatua katika kustawisha na kueneza harakati za Qur’ani miongoni mwa watu wa matabaka yote ya jamii hasa miongoni mwa watoto na mabarobaro.

3724024

captcha